Barua pepe (E-mail) ni njia nzuri sana ya kuwasiliana na inatumika sana katika kuwasiliana kibiashara. Ni vigumu sana kujua kama barua pepe yako imesomwa kama usipopata majibu ya aina yeyote kwa yule uliemtumia. Kama ulikua unaisubiria kwa hamu barua pepe kutoka upande wa pili alafu ukaona haiji lazima utakuwa na maswali mengi ya kujiuliza sio? Hilo sio tatizo tena kwani TeknoKona inakuja na maujanja mengine leo juu ya namna ya kujua kuwa email yako imesomwa au bado. Hii ina faida kwako kwa mara nyingine baada ya kukaa na kusubiria E-mail ya mtu unaweza endelea kufanya mambo mengine
Jinsi Ya Kuona Kama Barua Pepe Imesomwa
- Kwanza kabisa itabidi uongeze Extension ya MailTrack katika kivinjari chako cha Google chrome. Extension hiyo inaweza patikana kwa :-
- Nenda kwenye Settings za kivinjari chako cha chrome kisha chagua Extensions. Chini kabisa ya Extension zote ambazo zitajitokeza kwa chini yake kabisa kumeandikwa ‘Get More Extensions’ Bofya hapo.
- Ukurasa mwingine ukitokea chagua MailTrack na kisha bonyeza Enter
- Ukishafanya hivyo MailTrack itatokea kwa upande wa kulia, bofya Add to Chrome Extension Ya MailTrack
Ukishamaliza kuiweka katika kiivinjari chako, unaweza ukai ‘click’ MailTrack na baada ya hapo Window mpya itafunguka na kukuomba uingize Barua pepe yako. Hapo ndio inapokubidi uingize barua pepe yako ya Gmail. Kumbuka barua pepe hii uyoiingiza lazima iwe ile ambayo unataka kuona meseji kama zitakuwa zinasomwa au laa Kinachofuata itabidi uchague kifurushi unachotaka (kuna vifurushi viwili kila cha kulipia na kile cha bure) kwa sasa chagua cha bure tuu lakini hakitakuwa na vipengele vingi kama vile kile cha kulipia.
Aina Mbili Za Vifurushi Kile Cha Bure Na Cha Kulipia Ukishamaliza zoezi la kuchagua kifurushi, hapo unakuwa umemalizana na zoezi zima na utaweza kujua ni email zipi zimesomwa katika barua pepe zako za gmail kwa kutumia MailTrack. MUHIMU: Barua pepe yako ikisomwa utajua kwani katika eneo lako la sent utaona barua pepe hiyo ikiwa imepigwa tiki mbili (kama zile za WhatsApp) kuonyesha kuwa imeshasomwa
Alama Ya Tiki Ikionyesha Email Imesomwa
Pia utapata Notification katika sehemu ya Desktop katika kompyuta yako
Notification Katika Desktop
Fuatilia kwa undani ili kujua kama barua pepe zako ulizotuma katika
Gmail kama zimesomwa kwa kutumia ujanja huu (MailTrack) tuliokupa leo.
Je unaona hii ni sawa kujua kama barua pepe imesomwa katika Gmail au
laa? tupe mawazo yako sehemu ya comment hapo chini.TeknoKona Daima Tupo
Nawe Katika Teknolojia
Source;; techuntold