Mambo vipi rafiki?. Je umeshapata au
kusikia taarifa ya kufungwa kwa Simu feki, zilizoharibika, au kupotea ifikapo
Juni- 2016 na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Nimekuwekea maelezo ya
jinsi ya kutambua kama simu yako ni feki au Laa na njia za kufuata endapo
utatambua kifaa chako ni feki kabla ya siku husika haijafika.
Vifaa vya mawasiliano vya mkononi –
hususan simu za kiganjani na vifaa vya mawasiliano vya kiganjani (tablets) –
vina namba maalum inayovitambulisha. Namba hiyo inajulikana kama IMEI ambacho
ni kifupi cha International Mobile Equipment Identity.
Kifungu cha 84 cha Sheria ya
Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya 2010 kinataka kuwepo kwa mfumo
wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi. Rajisi
hii inajulikana kwa kiingereza kama Central Equipment Identification Register,
kwa kifupi CEIR. Sheria inataka rajisi hiyo ihifadhiwe na kuendeshwa na Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania.
Aidha Kanuni za mwaka 2011 za EPOCA
kuhusu mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya
mkononi inawataka watoa huduma wa mawasiliano yanayotumia vifaa vya mkononi
kuweka mfumo wa kudumu wa kumbukumbu za namba tambulishi (Equipment Identity
Register – EIR) za vifaa vya mkononi vinavyotumika kwenye mitandao yao.
Mfumo huu wa kielektroniki ambao
utahifadhi kumbukumbu za namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano vya mkononi
una lengo la kufuatilia namba tambulishi za vifaa vinavyoibiwa, kuharibika,
kupotea au ambavyo havikidhi viwango vya matumizi katika soko la mawasiliano.
Vifaa vyote vya mawasiliano vya
mkononi ambavyo vimeibiwa, vimeharibika, kupotea au visivyokidhi viwango vya
matumizi katika soko la mawasiliano havitaweza kufanya kazi kwenye mitandao ya
mawasiliano kutumia vifaa vya mkononi.
ifikapo
mwezi Juni mwaka 2016 kwa mjibu wa Taarifa zilizosamba.
Je
utaitambua vipi kama Simu yako ni feki au orijino kabla ujafungiwa?
Zifuatazo ni hatua unazoweza
kuzitumia kuangalia kama simu yako ni fake, hakuna mahitaji makubwa kufanya
hili ila tu unahitaji simu yako unayoitumia na unayotaka kuiangalia. Jinsi ya kuangalia
IMEI namba Andika *#06# kisha bonyeza kitufe cha kupiga Baada ya hapo simu yako
itakuletea IMEI namba ambapo kama simu yako au kifaa chako kina laini mbili
basi kutakuwa na IMEI namba mbili Namba hii pia unaweza kuipata katika boksi la
simu ama nyuma ya ya simu hiyo baada ya kutoa betri, utaijua kwa kuwa huwa ni
tarakimu 15. Nakili namba hizo pembeni.

Mfano wa IMEI namba iliyopatikana
kwa kupiga *#06#
Baada ya kuangalia kifaa kama ni
feki ama halali Iandike ile namba uliyo nakili katika hatua iliyopita katika
sehemu ya kuandikia ujumbe (SMS) Utume ujumbe huo kwenda namba 15090 Baada ya
kutuma meseji hiyo utaangaliziwa je hiyo IMEI namba ni ya simu ya aina gani na
nani mtengenezaji wa simu hiyo.
Subiri majibu (haitachukua muda
mrefu) Ujumbe huo ukija unakuwa na maelezo ya kampuni iliyotengeneza simu hiyo
pamoja na jina la simu hiyo.

Mfano wa ujumbe unarudishwa baada ya kutuma IMEI namba Jinsi ya kujua kama simu yako ni feki
Kama jina la mtengenezaji wa simu yako pamoja na aina ya simu yako (Uliyo jibiwa baada ya kutuma IMEI namba) haviendani na majina ya simu yako (ambayo yameandikwa katika simu yako) basi ujue simu yako inamashaka na ni vyema kumuuliza muuzaji wako juu ya hilo.

Mfano wa ujumbe unarudishwa baada ya kutuma IMEI namba Jinsi ya kujua kama simu yako ni feki
Kama jina la mtengenezaji wa simu yako pamoja na aina ya simu yako (Uliyo jibiwa baada ya kutuma IMEI namba) haviendani na majina ya simu yako (ambayo yameandikwa katika simu yako) basi ujue simu yako inamashaka na ni vyema kumuuliza muuzaji wako juu ya hilo.
Kama majina yaliyorudi hayaendani
na majina yaliyoandikwa katika simu yako basi upo katika kundi lenye uwezekano
wa kuwa na matatizo, Nakushauli ufuate utaratibu na kuibadilisha ama kuacha
kuitumia simu hiyo kabla ya mwezi Juni. Kwanini TCRA wanataka tubadilishe simu
Vyombo vya usalama vinaweza kukamata wahalifu wa kutumia mitandao ya simu kwa
msaada wa IMEI namba hivyo mtu akiwa anatumia simu ambayo haina au ina IMEI
namba ambayo sio sahihi anazuia utendaji kazi wa taasisi za usalama hivyo wao
kama mamlaka wanatakiwa kuhakikisha kila mtu anatumia simu yenye IMEI namba
sahihi.