Moja kati ya matatizo ya smartphones nyingi ni kuwa speed au kasi yake huwa ndogo sana. Hii hutokea mara nyingi kama umefungua applications/programs nyingi kwa mara moja. Je unawezaje kujikwamua na hali hii?
Kuna njia mbali mbali ambazo unaweza kutumia kuondokana na tatizo la simu kufanya kazi polepole. Njia kubwa na ya uhakika ni KUNUNUA SIMU YENYE UWEZO MKUBWA.
Hata hivyo kuna aina mojawapo ya simu ambayo ina uwezo mkubwa na gharama zake ni za kawaida. Hivi karibuni, kampuni ya uuzaji wa simu za mkononi kwa kushirikiana na Tigo wamezindua Huawei y360 ambazo zinauzwa kwenye maduka ya Tigo nchi nzima kwa shilingi 160,000. Pindi mteja anunuapo simu hizo, atarudishiwa pesa yote aliyonunua kama vifurushi mbalimbali kwa muda wa miezi sita.