
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw, Magessa Mulongo amemshutumu M/kiti wa Chama Cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bw, Freeman Aikael Mbowe kuwa ameongwa na mmoja wa waliyokuwa vinara wa kusaka Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili awe mgombea wa Urais kupitia chama hicho, pia aliongeza kuwa safari hii mkoa wa mwanza umejipanga sawa sawa kuwadhibiti wanasiasa wote watakao leta vurugu.
Mwishowe akasema kuwa CHADEMA kina Ukabila mbona uwa hawandamani Moshi kwao! namnukuu "kuna watu wanasema Dr Magufuri siyo Msukuma wakati Wenje ni Mjaruo na Kiwia ni Mchaga lakini wamechaguliwa na Wasukuma tutawashughulikia".
Haya yote kayasema katika sherehe za kuadhiamisha siku ya mashujaa zilizofanyika katika makutano ya barabara za Nyerere, Makongoro na Kenyatta.