Mbuga ya wanyama ya serengeti ambayo ni ya pili kwa ukubwa nchini Tanzania imechaguliwa kuwa kituo cha mbuga bora duniani kwa kushinda karibia mbuga 140 kutoka nchi 63 kote duniani.
Matokeo hayo yalitolewa katika ukurasa wa “Safari Booking” ambapo hufanya biashara za utalii katika mitandao ya kijamii.
Allan Kijazi, Mkurugenzi mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), aliiambia shirika la Anadolu kuwa kulikuwa na sababu kuu mbili za Serengeti National Park kuchaguliwa: "kila mwaka wanyama aina ya nyumbu zaidi ya milioni 2.5 na pundamilia wamekuwa wakihamia katika mbuga ya serengeti, na pia ni kituo ambapo wanyama aina ya simba na mamba kupatikana hapo.”