M-Pesa
bila ya shaka ni njia rahisi ya watu kutumiana pesa au kufanya malipo.
Facebook wanaanzisha mtindo mpya wa kutumiana pesa kupitia programu yao
ya jumbe ya Facebook Messenger itakayo muezesha mtumiaji kuunganisha akaunti yake na ile ya facebook.
Mfumo huo utaanzishwa nchini marekani kwa sasa na iwapo una kadi ya Visa au Mastercard utahitajika kubofa “$” kutuma pesa kwa umtakae kwenye mtandao wa facebook.
Facebook
wanahakikishia watumizi wake kwamba mtindo huo ni salama kwa kusema:
“Mbinu yetu ya malipo ni salama na inatumia miundombinu tofauti na
mtandao wetu wa Facebook ili kuhakikisha malipo yanafuatiliwa kwa
karibu.”
Pindi mtumizi atakapo ona alama ya “$” kwenyeMessenger yake, inamaanisha tayari yuko kwenye mtandao wa malipo ya Facebook.
Mtumizi
atafinya alama hio na kueka kiwango cha pesa kisha kubofa ‘tuma’ kama
anaetuma ujumbe. Pesa itatolewa moja kwa moja kutoka akaunti ya mtumizi
na kuzituma kwa akaunti ya anayetumiwa.
Mtu
atahitajika kueka maelezo zaidi kuhusu akaunti yake pamoja na kuwa na
neno la siri ili kuzuia mtu kueza kutuma pesa bila idhini ya mwenye
akaunti.
Mfumo
wenyewe utaanza kutumika nchini Marekani kwenye kipindi cha wiki chache
zijazo lakini unatarajiwa kuenea nchi nyengine duniani ambapo kutumiana
pesa itarahisishwa na kupunguza gharamaya ada zinazolipishwa kama
Western Union na Moneygram.