Aliyekuwa Mgeni rasmi katika uhamasishaji huo Mh Kassim Majaliwa ambaye ni Naibu Waziri wa Elimu ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI , akiwaelezea wakazi wa Masubwe Mkoani Geita, waliofika kwenye mkutano na kupatiwa elimu kuhusiana na kampeni ya kuelimisha wakina baba na wanachi kwa ujumla kuwaruhusu wakina mama wajitokeze ili wakatibiwe maradhi ya fistula bure katika hospitali ya CCBRT kwani yanatibika
Kampeni inayoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu –UNFPA, Kwa kushilikiana na CCBRT pamoja na Vodacom Foundation Ililipa jukumu Kampuni la Mpoto Theatre kueneza kampeini ya “FISTULA INATIBIKA”- Kwa kuhamasisha kuhusu athari na matibabu ya ugonjwa wa Fistula unaowapata wanawake baada ya kujifungua .
Madhimisho hayo yalihusisha Mikoa ya Geita (Masubwe) , Kigoma (Nyakanazi, Kibondo, Uvinza, Kasulu, na Nguruka), Tabora (Kalilia, Tabora mjini, Urambo, na Igunga) pamoja na Dododoma Mjini.
Hadi sasa matokeo ya kampeni hiyo yanazidi kuonyesha mafanikio kutokana na mwitikio wa jamii katika ushiriki wa mafunzo hayo sambamba na uwasilishwaji wa maswali kutoka kwa washiriki hao kuonyesha nia ya kufahamu juu ya ugonjwa huo.
Moja kati ya dalili za kuonyesha mwamko miongoni mwa jamii ni pamoja na njia ya uwasilishwaji wa ujumbe huo kutumia zaidi wasanii wa muziki na Burudani mbalimbali kama sarakasi na Maigizo jambo linalosaidia ujumbe huo kufika kwa haraka zaidi.
Katika kuakikisha ujumbe unawafikia wananchi kwa njia ya Sanaa Mpoto Theatre walitoa burudani mbalimbali na nzuri zaidi kama Muziki, Sarakasi pamoja na Maigizo katika Kampeini hizo.
Umati wa wakazi wa kata ya Masumbwe Mkoani Geita wakiwa kwenye
mkutano wa kampeni ya kutoa elimu kuhusiana na maradhi ya Fistula
yanayowakabili wanawake hapa nchini,Kampeni hiyo iliendeshwa na Hospitali ya
CCBRT kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania kupitia taasisi yake ya Vodacom
Foundation Pamoja na Mpoto
Theater Iliyofanyika katika mikoa mitatu kuwasisitiza wakina
baba kuwaruhusu wakina mama wajitokeze ili wakatibiwe maradhi hayo kwani
yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi
hayo wanapojifungua.