Header ads

Header ads
» » iPhone 6 yamulipukia wakati akiwasiliana

iPhone 6 yalipuka wakati wa mawasiliano

Ajali za milipuko ya simu zinazotokea zimeanza kuzua hofu miongoni mwa watumiaji wa Smartphones

Maboresho ya kiteknolojia kwenye miundo ya simu hasa ile michanganyiko ya kemikali zinazotumika kuunda betri, zinasemekana kusababisha betri kupata moto na kulipuka.
Mtu mmoja kwa jina la Kishan Yadav kutoka India, ameripotiwa kulipukiwa na simu yake ya iPhone 6 wakati alipokuwa akizungumza nayo.

Yadav alilipukiwa na simu hiyo ya iPhone 6 iliyotoa cheche za moto, baada ya kuzungumza nayo kwa muda mrefu.
Yadav alifahamisha kwamba simu hiyo ilimlipukia alipokuwa akizungumza ndani ya gari na kuirusha nje punde tu ilipoanza kuteketea.
Kampuni ya Apple iliyopokewa taarifa hizo, imechukuwa simu hiyo ya iPhone 6 kwa ajili ya ukaguzi, na kuamrisha maafisa wa usalama kuanzisha uchunguzi.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post