Baada ya nashindwa kuchukua mda wake kwenye radio station mbali mbali Christian Bella (king wa masauti ) anarudi tena na kazi nyingne akiwa amemshirikisha Alikiba
Akizungumza kwenye interview ambayo ilifanywa na Bongo5 Bella alisema
"Nimemfanya alikiba kuimba na Mimi na akaonyesha kiwango kingine baada ya kukaa na king wa masauti ,nilinyoosha melody na alikiba akatembea hivyo hivyo njia nilizopita Mimi ni pick za juu sana nae akaenda hivyo hivyo yani imekua nzuri sana, noma sana yani"
Bella pia aliongezea kwa kusema
"sasa hivi tunajipanga kwa ajili ya video na video ikimalizka baada ya kuisha kwa mwezi wa Ramadhani itatoka, sitaki ichelewe kwa sababu mashabiki wanasumbua wanataka nifanye kolabo na alikiba sasa umefika muda wao kupata walichokitaka ,ingawa imechukua mda mrefu hii ni kwa sababu ya sisi sote kuwa busy ,sasa kilichobaki ni video ili kutoa video na audio kwa pamoja video kwa ufupi itakua Kali na sidhani kama tutafanyia hapa nchini"
Mwimbaji huyo alisema pia bado hawajupa jina wimbo wao yeye na king kiba