JE mnachuliaje uamuzi alichokua Mbunge wa Muleba Kusini (CCM) na aliewahi kuwa waziri wa Ardhi nyumba na makazi,
Profesa Anna Tibaijuka jana baada ya kuzomewa mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, ambapo alisema haya
“Kama hamnitaki siyo lazima niwe mbunge wenu, mnaruhusiwa kubadili.
Huyo aliyewapa viroba asubuhi hii ili mje mnitie aibu mbele ya katibu
mkuu wa chama nawaambia hiyo dhambi itawatafuna,” alisema. “Mimi
sitafuti kazi na wala sina njaa... na kama hela ya kula ninayo. Mimi
sigangi njaa na kama mnataka kuwa na kiongozi mganga njaa muwekeni muone
atawasaidia vipi,”: