Binadamu wamepoteza utu!
Mwanamke mjamzito aliyefahamika kwa jina la mama Janeth, mkazi wa
Kimara-Suka jijini Dar anadaiwa kujifungua kisha kukiweka kichanga
kwenye begi na kukitupa shambani, kisa kikielezwa kuwa ni mgogoro wa
kimapenzi na mwanaume aliyempa ujauzito.
Mama anadaiwa kutupa kichanga hicho akijaribu kuangalia huku na kule kama kuna mtu anamuona alifahamika kwa jina la mama Janeth.
Mmoja wa mashuhuda
akizungumza na gazeti hili, alisema kichanga hicho kilikutwa na bibi
anayejulikana kwa jina la mama Joyce katika shamba lake lililopo eneo la
Moa, Kimara-Suka baada ya kubanwa sana mama Janeth alikiri kuwa ndiye
mwenye kichanga hicho.
Msamaria mwema akiangalia mfuko uliotupwa ukiwa na mtoto ndani.
Kufuatia kuulizana ndipo
mwenye shamba akakumbuka kuwa mama Janeth alikuwa mjamzito na
ilionekana alijifungua usiku, walipombana sana alikubali kukitupa
kichanga hicho.
Picha ya mtoto huyo alietupwa na mama yake aliefahamika kwa jiana la mama Janeth.
Ijumaa Wikienda
lilizungumza na mmoja wa mashuhuda ambaye hakutaka jina lake litajwe
alisema kuwa mama huyo alipohojiwa alisema mwanaume aliyempa ujauzito
aliukataa ndipo akaamua kufanya kitendo hicho.
Wananchi walifanikiwa
kumtia mikononi mama Janeth na kumhoji ila wakiwa wanajianda kuwaita
polisi, mwanamke huyo alichoropoka kiaina na kwenda kusikojulikana.
Baada ya polisi kufika
eneo la tukio, mama Janeth alikuwa kishatoroka na polisi wakalazimika
kuwachukua baadhi ya majirani kwa ajili ya mahojiano zaidi, huku mwili
wa kichanga hicho ukipelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Tumbi, Kibaha.
“Wanawake mnapaswa kuwa
makini sana katika suala la uhusiano kwani mnapokosea ndiyo chanzo cha
kupata ujauzito na mwisho mnawatupa watoto wenu, ” alishauri shuhuda
huyo ambaye hakupenda jina lake liwe wazi.