Zaidi wa wananchi 6000 wa kata ya wazo jimbo la kawe na kata ya goba jimbo la ubungo jijini dar es salaam hawana mawasilaiano ya barabara na huduma ya UMEME baada ya mto Tegeta kufurika maji na kusomba daraja lao la muda walilokuwa wanategemea kuvukia na kusababisha shughuli za kata hizo kusimama.
Wakazi hao wamethirika zaidi kutokana na mto huo kufurika maji
huku ukiendelea kulika ukizifuata nyumba za wananchi na wakazi wa mtaa
wa muungano waliopo kata ya goba na mtaa wa kilimahewa waliopo kata
wazo ambapo ITV imeshuhudia wakazi hao wakilazimika kuhatarisha maisha
yao kwa kutumia kamba kwa ajili ya kuvuka huku nguzo ya umeme mkubwa
ikiwa inaninyinia katikati ya mto huo Jambo lilolazimu shirika la ugavi
wa umeme nchini kakata huduma ya umeme katika kata hizo.
Wakizungumza na ITV wakiwa wamefatana na mwenyekiti wao wa mtaa wa
muungano wananchi hao wamewalaumu vingozi wao wakiwemo wabunge na
viongozi wa wilaya ya kinondoni kwa kutowawekea daraja la kudumu katika
mto huo na kuwasababishia adha kila mara mvua kubwa inaponyesha ikwemo
ya mwaka jana.
Wakazi wengine waliokubwa na mafuriko ni wanaoishi kandokando ya
mto mbezi ambapo nyumba zao zimesombwa na maji huku kingo za mto huo
zikiendelea kulika na kufuata nyumba zao ambapo wameiomba serikali
kuwapatia viwanja vya bei raisi sehemu nyingine.
Katika tukio lingine mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha
visima vya mafuta kujaa maji na kusababisha baadhi ya madereva wa vyombo
vya moto kukumbwa na adha kubwa ya magari yao kuzima baada ya kuwekewa
mafuta yalichanganyika na maji ya mvua katika kituo cha mafuta cha
kobil kilichopo afikana huku meneja wa kituo hicho akisuasua kuwalipa
madereva hao.