
Meli ikiwa inazama na ikiwa imezungukwa na mitumbw pamoja na boti ambazo zilisaidia kwenye uokoaji
Makaburi ya Igoma ambako ndugu zetu waliokuwa wakisafiri kwa meli ya MV Bukoba walizikwa.
RIPOTI ya Tume ya Jaji Robert Kisanga, iliyochunguza chanzo cha ajali ya mv Bukoba, inasema usiku wa kuamkia siku ya ajali, meli hiyo ilipakia abiria kati ya 750 na 800 pamoja nawafanyakazi 37.Kati ya hao 114 waliokolewa wakiwa hai wakati 391 waliokolewa wakiwa wamefariki na kuzikwa katika makaburi ya Igoma nje kidogo ya Jiji la Mwanza.
Miili mingine ilichukuliwa na ndugu na jamaa kuzikwa kwao pia Jumla ya miili 332 haikupatikana.Kila mwaka ifikapo Mei 21 watu mbalimbali wakiongozwa na viongozi wa dini na mbalimbali kwenda eneo la makaburi na kufanya maombi kwa ajili kumbukumbu ya ndugu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.
Serikali ilishitaki aliyekuwa nahodha wa MV Bukoba, Jumanne Rume-Mwiru (sasa marehemu), Mkaguzi wa Mamlaka ya Bandari Gilbert Mokiwa, aliyekuwa Meneja wa Bandari ya Bukoba Alphonce Sambo, na aliyekuwa Maneja wa Bandari ya Kemondo, Prosper Lugumila.Kesi hiyo Na. 22 ya mwaka 1998, ilianza kusikilizwa Mei 14 mwaka 2001.
Miongoni mwa waendesha mashitaka katika kesi hiyo ni Eliezer Feleshi,ambaye kwa sasa ni Jaji wa Mahakama kuu ta Tanzania.Hukumu ya kesi ilitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Juxton Mlay (sasa mstaafu), Ijumaa, 29 Novemba 2002, majira ya saa sita mchana.Washitakiwa wote walishinda kesi, kufuatia hukumu ya kurasa 118 iliyosomwa kwa dakika 160 na Jaji Mlay kusema, MV Bukoba ilizama kwa sababu haikuwa na uwiano wa majini na siyo uzembe wa washitakiwa.
Serikali iliahidi kukata rufaa lakini hadi leo majaliwa ya rufaa hiyo hayajulikani na baadhi yawashitakiwa wamefariki dunia bila kujua hatma ya kesi hiyo wala stahili zao.
Kwa kipindi kirefu MV Bukoba ilikuwa ‘kaburi’ lenye kuelea katika Ziwa Victoria. Ilikwishapigwamarufuku kufanya safari kwa kuwa haikuwa na viwango vya ubora wa kuwa majini.
Meli hii ilijengwa na kampuni ya Kibelgiji na ikazinduliwa 27 Julai 1979. Siku ya uzinduzi, ilibainika haikuwa thabiti kwani ilikuwa inakosa uwiano.
Uongozi wa Kitaani Bongo news Blog unatoa pole kwa nduguna jamaa waliopoteza wapedwa wao kwenye ajali ya meli ya MV Bukoba.
Topics: MATUKIO
Imehaririwa na;- Unknown
Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
Playstore
TeknoTaarifa Video
TAARIFA ZILIZOSOMWA SANA
-
Ingawa nipo Arusha,naendelea kudokezwa yanayochomoza vikaoni (ndani ya CCM) na katikati ya makada wa haja. Nimedokezwa kuwa CCM inaelekea ...
-
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ametangaza rasmi nia yake ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Waziri huyo amba...
-
KAMATI ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia (NBC) imeridhishwa na matumizi ya Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) yenye len...
-
Huu ndo ujio mpya Rehema Chalamila aka Ray C baada ya ukimya wa muda mrefu kwenye muziki amerudi rasmi na hii singl...
-
Hivi karibuni mdau mmoja wa Website hii alinitumia e-mail na kuniuliza ni kwa jinsi gani anaweza kuipata simu yake iliyo...
-
Kampuni moja ya Florida, Marekani imekuja na dhana ya kujenga meli ‘Freedom Ship’, itakayokuwa na uwezo wa kuwa na kila kitu ch...
-
Makala hii inakupa maelekezo ya mambo adimu katika kusimamia barua pepe zako, ili kuboresha ufanisi na- kufurahia kuwa na akaunti ya ema...
-
Kuna taarifa kuwa chanzo cha kifo cha ghafla cha rapper Mangweir ni kuzidisha madawa ya kulevya aliyotumia usiku wa kuamkia leo. Inadaiwa ...
Data Boosta