George Kirby mwenye umri wa miaka 103 na Doreen Lucky mwenye umri wa
miaka 91 watafunga pingu za maisha mwezi Juni tarehe 13 mwaka huu.
Kwa mujibu wa gazeti la Uingereza la Daily Mail, wapenzi hao walikutana
mwaka 1988 na tangu mwaka huo walikuwa hawajaamua kufunga ndoa.
Bwana harusi George alimposa mpenzi wake Doreen katika siku ya wapendanao.
George alipohojiwa kwa nini waliamua kuoana baada ya miaka yote hii
alijibu kuwa, “nadhani hata kama ningekuwa sijashtukia umri wangu, sasa
ndio wakati mwafaka wetu wa kufunga ndoa maana Doreen hunifanya nijihisi
kijana.”
Wanandoa hao waliongeza kuwa, “Hatukuchukuwa uamuzi wa kufunga ndoa kwa
ajili ya kuvunja rekodi yoyote ya dunia, bali kwa sababu tunapendana na
tumeona kwamba kufunga ndoa kwa wakati huu ndio hatua bora kwenye maisha
yetu.”