
Hama kweli ukistajabu ya Musa utaona ya Filaunu, SHIRIKA maarufu la Uchina, HAINAN
AIRLINE limeweka masharti kwamba mbali na elimu na uzoefu lazima usinuke. Ukiwa
mwili wako una harufu mbaya basi kazi huna. Ni China huko. Kwa mujibu wa gazeti
la SZ News shirika hilo katika kuajiri marubaNi wapya lazima mtu ananuswa
makwapa.Ukiwa unakikwapa, au makwapa yako yana harufu unanyimwa kazi. Kabla ya
kuajiriwa katika shirika hilo la ndege. Hatua ya kwanza ni kunuswa kwapa zako.
Wakuu wa shirika hilo wanajitetea wakisema, kwa vile marubani wanafanya kazi
karibu zaidi na watu basi ni lazima wasiwe na harufu ya kutisha kwani harufu
mbaya ya miili yao au makwapa huenda ikawapunguzia wateja.