Juzi, magaidi wa Al-Shabaab walifanya shambulio kubwa la ugaidi katika mji wa
Garisa, uliopo mpakani mwa Kenya na Somalia.Shambulio hilo limepelekea vifo vya watu takriban 150 huku taarifa mbalimbali zikionyesha uwezekano wa kuwepo idadi kubwa zaidi ya waliouawa. Awali, nilikuwa upande wa watetezi wa serikali ya Kenya na vyombo vya usalama vya nchi hiyo katika lawama kwamba walizembea kuchukua tahadhari.
Hoja yangu kuu ilikuwa kwamba kupewa taarifa kuhusu ugaidi ni kitu kimoja, kuweza kuzifanyia kazi taarifa hizo na kuweza kuzuia ugaidi ni kitu kingine kabisa.
Hata hivyo, utetezi huo umepungua baada ya kupatikana taarifa mbalimbali zinazoashiria mapungufu makubwa ya serikali ya Kenya na taasisi za Usalama nchini humo kukabiliana na tetesi walizopewa kuhusu uwezekano wa shambulio hilo la kigaidi.

Tukiweka kando kilichojiri nchini Kenya lakini tukitilia maanani ukweli kuwa nchi hiyo ilitahadharishwa kabla ya tukio hilo, kwa Tanzania hali ni tofauti. Hadi sasa hakuna taarifa rasmi ya uwezekano wa kutokea shambulio la ugaidi.
Hata hivyo, ni muhimu kutambua kuwa Kenya ina ushairikiano mkubwa zaidi na taasisi za kiusalama za mataifa makubwa zaidi ya Tanzania, hasa ikizingatiwa kuwa Marekani, kwa mfano, ina 'base' yake ya kijeshi nchini humo (Manda Bay)
Kwa maana hiyo, tahadharani ya Wamarekani kwa Kenya sio tu kwa maslahi ya Kenya bali ya Wamarekani pia.
Kwa kufanikiwa kufanya shambulio kubwa kabisa nchi Kenya, ikiwa ni takriban mwaka na nusu baada ya kufanya shambuli jingine la ugaidi kwenye supamaketi ya Westgate jijini Nairobi, magaidi wa Al-Qaeda wanaweza kushawishika kupanua kampeni yao ya uharamia hadi Uganda (ambako tayari kuna tishio kama ninavyoeleza hapo chini) na hata Tanzania (kwa sababu nitazobainisha mbeleni katika makala hii)
Uwezekano wa shambulio la kigaidi Uganda:
Machi 25 mwaka huu, Marekani ilitoa tahadhari kwa Uganda kuhusu uwezekano wa shambulio la kigaidi nchini humo.
Kama ilivyo kwa Kenya, Marekani ina maslahi yake nchini Uganda ambako inarusha ndege zake za upelelezi (PC 12) kutoka Entebbe, Kwahiyo usalama kwa Uganda una maslahi kwa Marekani pia.
Kama ilivyo kwa Kenya, Marekani ina maslahi yake nchini Uganda ambako inarusha ndege zake za upelelezi (PC 12) kutoka Entebbe, Kwahiyo usalama kwa Uganda una maslahi kwa Marekani pia.
Iwapo Al-Shabaab watafanikiwa kutimiza uovu wao kuishambulia Uganda (Mungu aepushe hili), wanaweza kupata motisho wa kutanua zaidi kampeni yao hadi Tanzania hasa kwa kuzingatia kuwa kundi hilo la kigaidi linaziona nchi hizi tatu kama kikwazo kikubwa kwa uhai wake.
Shaka ya ugaidi nchini Tanzania:
Moja ya matatizo makubwa ya kufahamu ukubwa au udogo wa tishio la ugaidi nchini Tanznaia ni siasa. Kwa muda mrefu, chama tawala CCM kimekuwa kikiutumia ugaidi kama kisingizio cha kudhibiti vyama vya upinzani na baadhi ya viongozi wake.
Kwa minajili hiyo, hata serikali ikitoa taarifa sahihi kuhusu uwezekano wa tishio la ugaidi, kuna uwezekano wa wananchi wengi kudhani hiyo ni siasa tu.
Kwa minajili hiyo, hata serikali ikitoa taarifa sahihi kuhusu uwezekano wa tishio la ugaidi, kuna uwezekano wa wananchi wengi kudhani hiyo ni siasa tu.
Kana kwamba hiyo haitoshi, mwaka huu Tanzania itafanya uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge hapo Oktoba. Japo haijazoeleka sana, historia inaonyesha kuwa angalau katika uchaguzi mkuu mmoja uliopita zilisikika taarifa za 'tishio la usalama' kutoka kwa nchi jirani.
Mbinu hii hutumiwa na vyama tawala kujenga hofu ya kiusalama kwa wapigakura, na kuwaunganisha chini ya mwavuli wa chama kilichopo madarakani.
Kwa mantiki hiyo, iwapo kutakuwa na taarifa za tishio la ugaidi, yayumkinika kuhisi baadhi ya wananchi wakatafrisi kuwa ni mbinu tu ya CCM kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.
Matumizi mabaya ya 'taarifa za kiintelijensia' yamewafanya Watanzania wengi kuwa na hisia kuwa 'taarifa za intelijensia' ni mbinu ya serikali kuwadhibiti.

Mara kadhaa,Jeshi la Polisi nchini humo limekuwa likipiga marufuku maandamano ya kisiasa au kijamii kwa kisingizio cha 'taarifa za kiintelijensia.'
Hivi karibuni, zilipatikana taarifa za mapigano makali kati ya jeshi la polisi wakishirikiana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) dhidi ya 'magaidi' kwenye mapango ya Amboni mjini Tanga. Mchanganyiko wa taarifa za kukanganya na imani haba ya wananchi kwa jeshi hilo vilipelekea tukio hilo kuonekana kama 'mchezo wa kuigiza.'
Tukiweka kando kasoro hizo hapo juu, hadi sasa kuna mambo yafuatayo ambayo yanaweza kuwashawishi magaidi kuvamia Tanzania.
1. Mgogoro wa muda mrefu kuhusu uanzishwaji wa mahakama ya kadhi:
Japo hadi muda huu suala hili limeendelea kuwagawa Watanzania kwa njia za mijadala na kwa amani, yayumkinika kuhisi kuwa magaidi wanaweza kulitumia kama kisingizio cha kuishambulia Tanzania.
Cha kutia hofu ni ukweli kwamba sio tu suala hili limedumu kwa muda mrefu, hasa baada ya chama tawala CCM kuahidi katika Ilani yake ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2005 kuwa itaanzisha mahakama hiyo lakini imeshindwa kufanya hivyo hadi leo, bali pia uamuzi usio wa busara wa kuupeleka Bungeni Muswada wa Uanzishwaji Mahakama ya Kadhi kisha kuuondoa.
Kana kwamba hiyo haitoshi, majuzi Rais Kikwete alikaririwa akidai kuwa serikali haina mpango wa kuanzisha mahakama hiyo, na badala yake jukumu hilo linabaki kwa Waislamu wenyewe. Haihitaji uelewa wa sheria kujiuliza kwamba kama suala hilo lilikuwa la Waislamu wenyewe, lilipelekwa Bungeni kwa minajili gani?
Licha ya mjadala huo wa uanzishwaji wa mahakama ya kadhi kuendelea kwa amani, mjadala kuhusu suala hilo umewagawa viongozi wa dini (Wakristo na Waislamu) na kwa kiasi flani umerejesha mgogoro kati ya baadhi ya viongozi wa Kiislam na serikali, sambamba na kuleta sintofahamu miongoni mwa baadhi ya wanasiasa.Japo hadi muda huu suala hili limeendelea kuwagawa Watanzania kwa njia za mijadala na kwa amani, yayumkinika kuhisi kuwa magaidi wanaweza kulitumia kama kisingizio cha kuishambulia Tanzania.
Cha kutia hofu ni ukweli kwamba sio tu suala hili limedumu kwa muda mrefu, hasa baada ya chama tawala CCM kuahidi katika Ilani yake ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2005 kuwa itaanzisha mahakama hiyo lakini imeshindwa kufanya hivyo hadi leo, bali pia uamuzi usio wa busara wa kuupeleka Bungeni Muswada wa Uanzishwaji Mahakama ya Kadhi kisha kuuondoa.
Kana kwamba hiyo haitoshi, majuzi Rais Kikwete alikaririwa akidai kuwa serikali haina mpango wa kuanzisha mahakama hiyo, na badala yake jukumu hilo linabaki kwa Waislamu wenyewe. Haihitaji uelewa wa sheria kujiuliza kwamba kama suala hilo lilikuwa la Waislamu wenyewe, lilipelekwa Bungeni kwa minajili gani?
2. Vitisho bayana kutoka kwa watu wanaodai ni magaidi.
Hivi karibuni ilipatikana video nchini Tanzania ambapo mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Kaisi Bin Abdallah alidai kuwa kundi lao limekuwa na mafanikio katika ugaidi wa kudhuru polisi na vituo vya polisi. Video hii chini inajieleza yenyewe.
Licha ya 'mapungufu kadhaa' katika video hiyo, ambayo yanaweza kutupa imani kuwa ni porojo tu, kwa kuzingatia nilichokitanabaisha mwanzoni mwa makala hii, yawezekana tishio lililo kwenye video hiyo ni la kweli. Na hili ni moja ya matatizo ya kukabiliana na tishio la ugaidi: kuchukulia taarifa kuwa ni serious au kuzipuuza.
Hofu kuhusu uwezekano wa matukio ya ugaidi nchini Tanzania ilithibitishwa na kauli ya hivi karibuni ya Rais Kikwete kuwa mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya vituo vya polisi katika maeneo mbalimbali nchini humo yana uhusiano wa ugaidi, japo hakubainisha iwapo kuna uhusika wa makundi ya kigaidi ya kimataifa au la
3. Taarifa za kimataifa:
Hadi muda huu hakuna taarifa za moja kwa moja zinazoashiria uwezekano wa tukio la ugaidi nchini Tanzania. Hata hivyo, bado kuna hali ya tahadhari wa wastani kuhusu uwezekano wa shambulio la kigaidi.
Wakati serikali ya Canada inaeleza kuwa haina 'ushauri unaohusu taifa (Tanzania) zima, inawashauri raia wake kuchukua tahadhari kubwa kuhusiana na ugaidi.
Kwa upande wake, Serikali ya Uingereza inatoa angalizo la jumla tu japo inatahadharisha kuhusu tishio la ugaidi wa Al-Shabaab kwa eneo la Afrika Mashariki (ikiwa ni pamoja na Tanzania). Serikali ya Marekani inatoa ushauri wa jumla tu kwa kurejea matukio ya uvunjiafu wa amani huko nyuma.
Hata hivyo, ripoti iliyotolewa LEO na taasisi ya HTH Worldwide kuhusu risks zinazoikabili Tanzania, ugaidi unatajwa kuwa ni tishio la kuaminika, japo uwezekano wa kutokea shambulizi la ugaidi ni wa wastani.
Pengine taarifa ya kuogofya zaidi ni ile iliyobainisha uwepo wa jitihada za kundi la kigaidi la ISIS kutaka kujiimarisha katika eneo la Afrika Mashariki, ikiwa ni pamoja na Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ISIS inajaribu kujenga ushirikiano na Al-Shabaab kwa minajili ya kuwa na infulence katika eneo la Afrika Mashariki.
Kadhalika, majuzi zimepatikana taarifa kutoka Kenya kuhusu mwanamke mmoja wa Kitanzania aliyekamatwa na wenzie wawili Wakenya wakijaribu kwenda Somalia kuwa wenza wa magaidi wa Al-Shabaab.
Tukio hilo linaakisi kinachotokea katika nchi mbalimbali za huku Magharibi ambapo mabinti kadhaa wamekuwa wakitorokea Syria kwenda kuwa 'wenza' wa magaidi wa ISIS.
Hitimisho:
Ni vigumu kwa kuwa na hakika ya asilimia 100 iwapo magaidi watafanya shambulio au la. Kwa upande mmoja, magaidi wana muda wote wanaohitaji kabla ya kutimiza azma yao, yaani wanaweza kusubiri kwa muda mrefu, ilhali vyombo vya dola havina faida hiyo kwani vinatakiwa kuwa makini muda wote.
Kuna msemo maarufu kuhusu ugaidi, kwamba wakati magaidi wanahitaji DAKIKA MOJA TU kutimiza uovu wao, vyombo vya usalama vinahitaji KILA SEKUNDE YA DAKIKA kuwazuwia magaidi husika.
Na japo uwepo wa taarifa za uhakika kuhusu uwezekano wa shambulio la kigaidi unaweza kusaidia jitihada za kukabiliana na magaidi husika, ukweli mchungu ni kwamba, kuwa na taarifa ni kitu kimoja, uwezo wa kuzitumia taarifa hizo ni kitu kingine.
Wakati huu tunaungana na wenzetu wa Kenya kulaani unyama wa Al-Shabaab, ni muhimu kuchukua tahadhari mahususi ili kuweza kukabiliana na uwezekano wa magaidi hao kushambulia Tanzania.
La muhimu zaidi ni umoja na mshikamano, ambao kwa hakika unapotea kwa kasi, na haja ya haraka kwa Serikali kurejejesha imani ya wananchi kwake. Kingine ni umuhimu wa kuweka kando siasa katika masuala nyeti kama haya..
Kubwa zaidi ya yote ni la kitaalamu zaidi. Wakati serikali ya Tanzania imekuwa ikitegemea zaidi msaada wa kimataifa katika kuiimarisha kiuwezo Idara ya Usalama wa Taifa, ni muhimu jitihada za ndani pia zielekezwe katika kuijengea uwezo wa kukabiliana na matishio mbalimbali ya usalama wa taifa, ikiwa ni pamoja na ugaidi.
Kwa uelewa wangu, uwezo wa vitengo vya kuzuwia ugaidi na kitengo cha kupambana na ujasusi unaathiriwa na mapungufu ya kimfumo na kisera, sambamba na nafasi ya maafisa wa Idara hiyo kwenye balozi za Tanzania nje ya nchi 'kubweteka' na teuzi zinazodaiwa kufanywa kwa misingi ya undugu,urafiki au kujuana.
Mwisho, tishio la ugaidi sio la kufikirika. Lipo, na kwa bahati mbaya, mazingira ya kulirutubisha tishio hilo yapo pia.
Imeandikwa Na Evarst Chahali.