Mkulima mmoja nchi Kenya anasema kuwa mmoja wa ng'ombe wake amesusia lishe yake ya kawaida na kuanza kuwala kondoo.
Charles
Mamboleo, ambaye anamiliki shamba kusini magharibi mwa kaunti ya Nakuru
aligungua kuwa ng'ombe wake amemla kondo siku moja asubuni.Jitihada zake za kumpa ng'ombe huyo chakula na maji hazikufua dafu, na siku iliyofuata ng'ombe huyo alimla kondoo mwingine.
Kulingana na afisa mmoja wa kilimo ni kuwa , huenda tabia ya ng'ombe huyo huenda imetokana na ukosefu wa madini yanayopatikana kwa mimea mbichi.
Hali ya kiangazi ambayo ilimalizika hivi majuzi huenda imesababisha mifugo kukosa madini yanayopatikaan kwenye nyasi mbichi. Mwaka 2007 ndama mmoja nchini India alinaswa kwenye mkanda wa video akila kuku.