Nikawaza sana juu ya upotevu wa pesa yangu, nikajiuliza inakuwaje mtu ufanye matumizi ya pesa ndotoni? Likanijia wazo kuwa yule binti si mtu wa kawaida. Nikajishauri kwenda kupata ushauri kwa rafiki yangu wa karibu. Wakati natoka kwenye chumba changu kuna sms ikaingia kwenye simu yangu ila nikaipotezea sikuisoma wala nini.
Nikaenda kwenye shughuli zangu, badae nikaenda kwa mshikaji wangu kumweleza kama nilivyowaza. Nikamkuta na tukapiga story mbili tatu badae nikamweleza mambo yote.
MIMI: Ndio hivyo bhana.
RAFIKI: Aaah pole sana mshikaji wangu ila nilikwambia kuwa makini na Tanga, hata hivy usipende kuwatongoza mademu hovyohovyo sehemu yoyote ile.
MIMI: Sasa nishauri ndugu cha kufanya.
RAFIKI: Cha msingi tumtafute mtaalam twende, haya mambo ya kishirikina kaka.
MIMI: Dah umenitisha kaka hata kurudi kwangu naogopa.
RAFIKI: Usiogope wangu, wee nenda tu ukiogopa atakushtukia mapema.
MIMI: Dah sijui kama nitalala leo kaka.
RAFIKI: Usijari kaka, cha msingi potezea kama hujui kitu vile halafu kesho twende kwa mtaalam kaka.
MIMI: Poa kaka nashukuru maana nishapagawa hapa.
Tukaagana pale halafu nikarudi kwangu.
Nikiwa chumbani nikachukua simu yangu kuikaguakagua nikakuta missed call kibao na sms moja nikashangaa hata ilikuwaje sikusikia wakati inaita, kumchek aliyekuwa anapiga ni demu wangu wa Dar na ile sms ni kutoka kwa binti wa kitanga, iliandikwa "usijaribu kumweleza yoyote juu ya habari zangu" nikashtuka sana, ni hii sms niliyoipotezea wakati naondoka asubuhi. Mara simu ikaanza kuita, kuangalia ni dada yangu anapiga
MIMI: Hallow dada,
DADA: Mbona umekuwa na akili fupi sana wewe? Unajua matatizo aliyoyapata mchumba ako huku?
MIMI: Kwani kafanyeje tena dada?
DADA: Muda wote amekupigia simu hupokei, mwenzio yupo hoi huku ule ujauzito umetoka.
MIMI: (Hata nilisahau kama demu wangu wa Dar alikuwa na mimba yangu) nini dada mbona sikuelewi?
DADA: Huwezi kunielewa kwa simu, kama unaweza njoo hospitali au njoo nyumbani.
MIMI: Poa dada ngoja nijiandae.
Nikakata simu, nikaenda kuoga na kuvaa fastafasta niondoke, wakati nataka kutoka simu yangu ikaanza kuita, kuitoa na kuiangalia ni yule binti wa kitanga.
BINTI: Unataka kwenda wapi?
MIMI: Aaah hapana siendi popote.
BINTI: (Akacheka kidogo), unataka kwenda wapi?
MIMI: Eeeh aaah nataka kwenda kutafuta chakula.
BINTI: Haya rudi kakae, chakula nitakuletea leo.
MIMI: (Huku nikiwa na hofu moyoni), utaniletea kivipi?
BINTI: Kwani shida yako ni chakula au ni nini? Kama ni chakula sasa mashaka ya nini si nimekwambia nitakuletea au?
MIMI: (nikaamua kujigeresha kidogo), aaah Acha utani bhana mpenzi wangu, unajua wazi upo mbali sasa chakula utakiletaje?
BINTI: Nitakileta kwa hisia na utashiba kabisa kwahiyo usitoke.
Akakata simu, nikaanza kuwaza itakuwaje sasa na vipi kuhusu kwenda hospitali nikawaza cha kufanya, au niende halafu akipiga nimwambie sijaenda? Bado nikawa na utata moyoni. Nikainuka pale nilipokaa na kujipa moyo kuwa naenda tu hata iweje. Nikaenda mpaka mlangoni ile nataka kufungua mlango tu sms ikaingia kwenye simu yangu, kuangalia ni demu wa kitanga "nimekwambia usitoke"
ITAENDELEA