Mkurugenzi
Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig. Jen.
Mbazi Msuya akioneshwa na Kiongozi wa Matengenezo wa Kampuni ya
kuzalisha umeme M&P mkoani Mtwara, Musa Kongola, eneo lililoathiriwa
na mvua karibu na kiwanda hicho kwa kusababisha udongo kushuka zaidi ya
mita mia kutoka usawa wa bahari
Eneo
la nchi kavu ambalo udongo umeshuka zaidi ya mita mia kutoka usawa wa
bahari, karibu na bomba la kusafirisha gesi na kiwanda cha kuzalisha
umeme cha M&P Mnazi bay Msimbati Mkoani Mtwara.
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa shughuli za Kuratibu Maafa, Brig. Jen, Mbazi
Msuya akikagua maafa yaliyosababishwa na mvua katika kalvati la
barabara ya mbae inayounganisha vijiji vya Mbae na Mbawala, Mtwara
Mikindani, Aprili 2015.(katikati) ni Mhandisi msaidizi wa Halmashauri
hiyo, Is-haka Mpaki
Sehemu
ya Barabara ya Mbae ambayo kalvati lake limebomolewa na mvua, barabara
hiyo inaunganisha vijiji vya Mbae na Mbawala, Mtwara Mikindani.
Mkurugenzi
wa Idara ya Kuratibu shughuli za Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig.
Jen. Mbazi Msuya akiwaonesha viongozi wa Kampuni ya Kuzalisha umeme
mkoani Mtwara M&P jinsi ya kuzuia udongo usishuke zaidi kutoka usawa
wa bahari.
Muonekano
wa Alama lilipo bomba la kusafirisha gesi, Kiwanda cha kuzalisha umeme
cha M&P na sehemu ya nchi kavu ambayo udongo umeshuka zaidi ya
kilomita mia kutoka usawa wa bahari katika eneo la Msimbati Mkoani
Mtwara