Majambazi wa nchini El Salvador wakihamishwa kutoka gereza la Izalco kwenda gereza la San Francisco Gotera
Uongozi
nchini El Salvador wamehamisha wafungwa kutoka kwenye magenge mawili na
kuwaingiza kwenye gereza moja kwa mara ya kwanza, ili kuwazuia
wasifanye shughuli wakiwa gerezani.
Hawa ni majambazi wa genge la Barrio 18
Picha
za ajabu inaonyesha wamefungwa pingu kutoka kwenye genge maarufu Barrio
18 wakiongozwa kuingia kwenye basi kutoka kwenye gereza la Izalco
kwenda San Francisco Gotera katika jitihada za kupambana na uhalifu.
Wakiwa wamefungwa pingu kwa namna yake
Wanachama 1,177 wa genge la Barrio 18 walihamishwa.
Majambazi hao walichanganywa na mahasimu wao
Na hawatawekwa pamoja kutokana na magenge yao, bali kwa uhatari wao.
Majambazi hawa wanahusika na mauaji ya polisi 20, wanajeshi wawili, askari magereza sita na mwendesha mashtaka
Sera
ya kuchanganya magenge pamoja ilikuja wakati maafisa walipogundua kuwa
magenge yalikuwa yakielekeza shughuli za uhalifu kutokea gerezani.
Majambazi hawa wamekuwa wakiendesha uhalifu ilhali wapo gerezani
Januari, uongozi wa serikali ya El Salvador waliagiza polisi kuwapiga risasi majambazi hawa bila woga wowote
Majambazi wa Berrio 18 wakishuka kwenye basi
Jambazi akiwa amepozi katika gereza la Izalco mwaka 2013
Mfungwa wa genge la Mara 18 akiwa amepozi gereza la Izalco Mei 20, 2013
Mfuasi wa genge la Mara Salvatrucha akiwa nchini Honduras 2006
Kiongozi wa zamani wa Mara Salvatrucha akiwa Honduras 2008