Ziona Chana anaishi na wake zake wote katika jengo lenye vyumba 100. Wake zake hufanya zamu kulala naye.
Hutumia jumla ya kuku kutengeneza chakula cha usiku.
Yeye ni mkuu wa familia kubwa zaidi duniani - na anasema kuwa 'amebarikiwa' kuwa na wake 39.
Vile vile, Ziona Chana ana watoto 94, - wakwe 14 na wajukuu 33.
Wanaishi
katika nyumba yenye vyumba 100, yenye ghorofa nne ambayo imejengwa
katikati ya vilima vya kijiji cha Baktwang katika jimbo la Mizoram
nchini India, ambapo wake zake hulala katika vyumba vikubwa vya pamoja.
Bw. Chana aliliambia gazeti la the Sun: 'Leo ninajihisi kama mtoto maalumu wa Mungu. Amenipa watu wengi kuwatunza.
'Ninajiona kama mwanaume mwenye bahati kwa kuwa mume wa wanawake 39 na kiongozi wa familia kubwa kabisa duniani.'
Familia
hiyo inaendeshwa kwa nidhamu ya kijeshi, ambapo mke mkubwa Zathiangi
huwasemamia na kuwapanga wenzake kufanya kazi za nyumbani kama vile
kufanya usafi, kufua na kuandaa chakula.
Katika mlo mmoja wa jioni hutumia kuku 30, humenya lb 132 za viazi na kupika kilo 220 za mchele.
Wakati huo huo, Bw. Chana pia ni kiongozi wa madhehebu ya dini inayowaruhusu wafuasi wake kuoa wake wengi anaowataka.
Alioa
wanawake kumi katika mwaka mmoja, wakati wa ushababi wake, na hulala
katika jumba cha pekee yake chenye kitanda kikubwa huku wake zake
wakilala katika vyumba vya pamoja.
Wanawake
vijana zaidi huwaweka jirani na chumba chake huku wale wakongwe
wakilala vyumba vya mbali - na kuna mfumo wa mzunguko kwa wale wanaolala
naye.
Rinkmini,
mmoja wa wake wa Bw. Chana, ambaye ana umri wa miaka 35 anasema:
'Tunakuwa karibu naye kwa sababu ndiye mtu muhimu zaidi katika famiia.
Ndiye mwanaume mzuri na mwenye mvuto kuliko wote kijijini.
Mwanamke
huyo anasema kuwa Bw. Chana alimuona akitembea kijijini asubuhi moja
miaka 18 iliyopita, akamuandikia barua ya kutaka kumuoa.
Mke
wake mwingine, Huntharnghanki, alisema kuwa familia yote inaishi
pamoja. Inaelezwa kuwa familia hiyo inaishi kwa mfumo wa 'kupendana na
kuheshimiana'
Naye Bw Chana, ambaye madhehebu ya dini yake ina wafuasi 4,00, bado anaendelea kutafuta wake wapya.
'Ili kupanua dini yangu, niko tayari kwenda hata Marekani kwa ajili ya kuoa,' alisema.
Mtoto
wake mmoja alisisitiza kuwa Bw Chana, ambaye babu yake alikuwa na wake
wengi, huoa wanawake maskini wa kijijini hapo ili apate kuwatunza.