muuaji (kulia)akiwa na wapelelezi nani ya pingu |
KUUA kwa shuku ya uchawi kumefanyika nchini Uingereza kwa babu mmoja mwenye miaka 73 kumtia nyundo mwenzake mwenye umri wa 77.
babu huyo Alan Rogers baada ya kufanya mauaji hayo aliwapigia simu Polisi na kuwaambia amemuua jirani yake Fred Hatch kwa kuwa anatumia uchawi kudhuru watu wengine.Wote hao ni wakazi wa Fair Oaks , Dinas Powys, Vale of Glamorgan.
Wakati akikamatwa na kutiwa pingu aliwaambia polisi kwamba amesubiri muda mrefu kumuua jirani yake huyo kwa kuwa ni mchawi.
Rogers amekiri kufanya mauaji asiyokudia alipofikishwa mahakama ya Cardiff Crown Court, ambayo pia imekubali kwamba na alikuwa na utata katika afya ya akili yake wakati alipomshambulia Hatch. ugonjwa huo kwa kizungu unaitwa paranoid schizophrenia.
Hata hivyo jaji Warby amemhukumu kuwa chini ya uangalizi wa watabibu maisha yake yote ili asidhuru wengine.