Kwa takribani kipndi kama cha mwezi mzima uliopita kumeibuka msuguano mkubwa sana hasa kwenye mitandao ya kijamii kati ya wafuasi wa CHADEMA dhidi ya wafuasi wa chama cha ACT.
Msuguano huo hasa unahusisha wale wafuasi wa CHADEMA kurusha tuhuma nzito dhidi ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA ndugu Zitto kwa kumuita -------, Anatumiwa na CCM kuuwa upinzani, Anaandaliwa mikutano yake na CCM na shutuma nyinginezo nyingi nyingi tu sina haja ya kuzirudia hapa.
Lakini kwa upande wa huyo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA yeye alishapigia mstari kule alikokuwepo na ameanza safari yake mpya katika chama kipya na ambacho amakiasisi yeye mwenyewe wakati akiwa bado na kesi dhidi ya CHADEMA na hatukuwai kumsikia ama haijathibitishwa ya kwamba huko ACT alipohamia amekuwa akiwatuhumu ama kuwashambulia viongozi wa chama chake cha zamani lakini pia chama chake cha zamani.
Sasa nirudi katika hoja ya kwanini Mbowe, Slaa na baadhi ya wanachama wa chadema walio watiifu kwa Mbowe na wale wafuata mkumbo wanahofu dhidi ya ZITTO?
Ni ukweli usiopingika Mbowe na Zitto ndio waliotumia muda mwingi kukijenga chama hicho na kuwaaminisha Watanzania kwamba muarubaini wa matatizo yao umepatikana na katika pilika za kukujenga chama hicho ndugu Zitto aliwavutia vijana wengi sana kuipenda siasa hasa ikizingatiwa kipindi kile hakukuwa na vijana waliokuwa wanavutiwa na siasa.
Kwa mantiki hiyo ndani ya CHADEMA kuna viongozi wengi ambao wamekuwa wakinungunika muda mrefu sana kutokana na aina ya uongozi wa mabavu ambao mwenyekiti na katibu wake pamoja na wale vipenzi vyao wanaoutumia.
Na wamekuwa hawana sehemu ya kusema kwa kuwa wako ndani ya chama lakini wametengwa na ni wanamageuzi wa ukweli kabisa nikiwa na maana hawawezi kuhamia chama tawala kwa hiyo wamekuwa kwa muda mrefu wakivumilia vurugu zote na mabavu ya Mwenyekiti na genge lake.
Sasa hofu inakuja zaidi kwa Mwenyekiti na genge lake kwa kuwa wale Makamanda sasa wanamahali pakuelekea na hasa baada ya kuona mwanzo wa ziara za ACT na hali yakuwa Makamanda hao wanaushawishi mkubwa sana katika jamii inayowazunguka.
Wasalaam
Topics: MATUKIO
Imehaririwa na;- Unknown
Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
Playstore
TeknoTaarifa Video
TAARIFA ZILIZOSOMWA SANA
-
THE UNITED DEPUBLIC OF TANZANIA MINISTRY OF HOME AFFAIRS EMPLOYMENT OPPORTUNITIES The Ministry of Home Affairs in clos...
-
Wakati CCM ikifanya jitihada za kudhibiti makada wake wanaotajwa kuwania urais, Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal amemtuma waziri ...
-
The Benjamin William Mkapa HIV / AIDS Foundation (BMAF) is a Trust and not for profit organization with a vision to be a hub of in...
-
The National Examinations Council of Tanzania (NECTA) is a Government Institution which is under the Ministry of Education and Vo...
-
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo kilichowekwa kanisani wakati wa mazishi ya kada mkongwe wa CCM Mzee...
-
Ref. Na EA.7/96/01/H/ 66 07th August, 2015 VACANCIES ANNOUNCEMENT On behalf of Eastern Africa Statistical Training Centre ...
-
Regional Manager. TANROADS - RUVUMA is looking for suitable qualified Tanzanian candidates for 11 posts available at Luhimba and...
-
Miaka miwili baada ya India kuzindua Nirbheek,bunduki inayodaiwa kuwa ya kwanza ya wanawake,kiwanda cha kutengeza silaha cha taifa hi...
Data Boosta
