Header ads

Header ads
» » Prof. Tibaijuka ziarani Muleba Kusini, asafiri kwa bodaboda umbali wa kilomita 13

 
Mbunge wa muleba kusini Prof Anna Tibaijuka alitembelea kata ya kimwani kijiji cha kaguramo kitongoji cha kaazi nyakishabo na kulakiwa namamia ya wananchi waliopanda mlimani wakiwa na matawi ya miti huku wakiimba. Kaazi ni kambi kubwa ya wavuvi


Mwenyekiti wa kitongoji cha Kaazi Nyakishabo Ndugu Ojax Dorolyma Lyapa alionyesha furaha yake kwa kusoma risala ya kijiji kwa lugha ya kimombo huku akishangiliwa alipokuwa anaitafsiri. Mwenyekiti huyo alisema ProfTibaijuka ametengeneza historia kuwa Mbunge wa kwanza tangu uhuru kufika kwenye kijiji hicho kilicho mwambao wa ziwa.

Prof Tibaijuka aliwasili Kyota majira ya saa 11 jioni akiwa amechelewa akitokea Bukoba ambapo alilazimika kuhudhuria kikao cha kamati ya siasa ya mkoa ya chama cha mapinduzi ambamo yeye ni mjumbe.
Kwa ubovu wa barabara Prof aliacha gari yake Kyota na kupanda pikipiki kilometa 13 hadi kaguramo mwisho ambapo alishuka na kutembea kilometa 2 kutelemka mlima mkali hadi Kaazi Nyakishabo.






Alishuhudia mamia ya watoto wa shule ya msingi wanaolazimika kutembea kilometa 7 kila siku kwenda shule ya msingi kaguramo.

Mwenyekiti wa kijiji aliomba prof tibaijuka akubali kufadhili ujenzi wa shule ya msingi itakayojulikana kwa jina lake kijijini hapo. Bila kumungunya maneno mwenyekiti huyo wa ccm alimtaka prof kuendelea na ubunge wa jimbo hilo kuleta maendeleo.

Prof alianza hotuba yake kwa kuwataka watoto wasiokwenda shule kijitokeza. Mtoto Abdu akaja mbele na kusema ameacha darasa la 3 kwa kukosa sare ya shule. Papo kwa papo prof tibaijuka alitoa fedha za kumshonea sare. Prof pia akachanga lhakib 2 na nusu mfuko kuwasaidia watoto wahitaji waendelee na masomo. Prof akaafiki kushirikiana na wanakijiji kujenga shule ya msingi baada ya kuambiwa kijiji cha nyakishabo kina kaya 400. Prof alisema atawasiliana na Halmashauri kuhusu suala hilo.

Mwenyekiti wa kijiji aliorodhesha kero ya umeme barabara na prof akaafiki na kuahidi kuzifanyia kazi. Prof alitoa michango mbalimbali kwa vikundi vya wanawake na vijana waliosoma risala zao jumla milioni mbili na nusu.

Mkutano wa Kyota uliahirishwa kwa usiku kuingia hata hivyo prof aliwasalimia wananchi wsliomdubiri hadi usiku na kuahidi kurejea siku nyingine.

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post