Watu
watatu wamefikishwa mahakama ya wilaya ya Chato kusomewa shitaka la
mauaji ya mtoto Yohana Bahati aliyeibiwa hatimaye kuuwawa tarehe 15
Februali katika kitongoji cha mapinduzi wilayani Chato mkoani Geita.
Akizungumza
na waandishi wa habari, kamanda wa polisi mkoa wa Geita Sacp Joseph
Konyo amesema watu wengine wawili bado wanahojiwa na jeshi la polisi ili
kupata ushahidi unaojitosheleza katika kesi hiyo, amewataja watu
waliofikishwa mahakamani ni Bahati Misalaba ambaye ni baba wa Yohana,
Juma Lupembe Kilebelo, Manyanda Mandege almaarufu Makongoro mkazi wa
wilaya ya Mbogwe na mchimbaji wa dhahabu.
Kamanda
konyo amesema jeshi la polisi linaendelea na juhudi za kuwakamata
wauwaji wa kukodiwa wanaofanya mauaji hayo kwa ujira mdogo wa laki moja
ili kudhibiti vitendo vya mauaji katika maeneo ya kanda ya ziwa.
Katika
tukio jingine jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata na kuwafikisha
mahakamani watu watatu wanaosadikika kuwa ni majambazi wazoefu wa kuteka
magari barabarani na kuvamia maduka ya fedha mkoani Geita, watu hao
Niosca John Bosco, Kapuru Msigwa ustaadhi, na Elias Shigilimelo Bambala.