Header ads

Header ads
» » Chimbuko la utajiri wa Lowassa hili hapa. Je, anafaa kuwa rais?




Leo nitaanika hapa waziwazi chimbuko la utajiri wa moja ya wanasiasa ambao wamekuwa wakitajwa sana kuwa wanafaa kuongoza nchi yetu katika nafasi ya urais. Mwanasiasa huyo akiwa ni mhe. Edward Lowassa au maarufu kama "Mamvi".

Mhe. Lowassa ambae ni mbunge wa jimbo la Monduli aliweza kujilimbikizia mali nyingi za umma katika kipindi kifupi kwa njia ambazo SIO halali.

Wengi mtakuwa mnajiuliza ni lini na wapi mhe. Lowassa alipata mali zake?

Jibu ni, alivyokuwa waziri anayesimamia kitengo cha maafa. Itakumbukwa kuwa mnamo miaka ya 90 Tanzania ilikumbwa na mvua kubwa zilizosababisha maafa kwa wananchi wengi. Na kwa kuwa Lowassa ndiye alikuwa akisimamia kitengo tajwa, hivyo alitumia madaraka yake hayo vibaya kujibebea misaada ya aina mbalimbali kutoka kwenye mashirika, taasisi na wasamalia wema waliotoa misaada yao kwa waanga wa majanga yale ya mvua za elnino.

Hilo ni moja, lakini pia mhe. Lowassa ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa JMT, kipindi akiwa mkurugenzi mkuu wa AICC, alitumia madaraka yake hayo kutoa tenda za upendeleo kwa kampuni zinazofanya plumbing za majengo ya kituo hicho cha kimataifa cha mikutano. Jambo ambalo Lowassa alifaidika nalo ni kujengewa nyumba na kampuni hizo kama aksante maana tenda zilikuwa zina thamani ya mamilioni (miaka ya 90).

Mhe Lowassa pia alivyokuwa wizara ya mifugo katika awamu ya Mkapa, alitumia nafasi yake hiyo kujimilikisha "Ranchi" za mifugo na kuhodhi maeneo makubwa ya ardhi, ambayo baadae aliyakodi kwa wazungu kwa gharama kubwa zaidi.

WanaJF, hii ni episode 01 ya umafia wa Lowassa katika kujijenga kiutajiri. Nitaleta episodes zake zingine kuonyesha ni jinsi gani Lowassa alinufaika katika kipindi cha sera ya ubinafsishaji. Ngoja nikuache kwanza ukiendelea kutafakari juu ya uhalali wa mjanja huyo wa kimasai kuongoza nchi katika nafasi ya urais.

Utajiri wa Lowassa ni ng'ombe zaidi ya 800 na nyumba ya kuishi basi

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post