Askari
wa jeshi lapolisi, Sajenti Patrick Kondwa amejiua kwa kujipiga risasi
akiwa katika ofisi yake kwenye ghala lakuhifadhia silaha katika kituo
cha polisi cha wilaya ya mbozi mkoani mbeya.
Akizungumza
na ITV kwanjia ya simu, kamanda wa polisi mkoa wa mbeya amekiri kutokea
kwa tukio hilo na kusema kuwa chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika
na kwamba jeshi lapolisi linaendelea na uchunguzi wa tukiohilo.
Sajenti
Patrick mwenye umri wamiaka 54 ,akiwa katika ofisi yake kwenye chumba
cha kuhifadhia silaha katika kituo cha polisi cha wilaya ya mbozi
amejipiga risasi mdomoni ambayo imetokea kisogoni na kuondoka na uhai
wake, tukio ambalo limetokea majira ya saa tisa usiku na kuthibitishwa
na kaimu mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo,
ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya ileje, Rosemary Staki Senyamule.
Baadhi
ya waombolezaji ambao wamezungumza na ITV wamesema kuwa wamepokea
msiba huo kwa masikitikomakubwa hasa kwa kuzingatia kuwa Sajenti Patrick
alikuwani askari mwadilifu na anayeipenda kazi yake.
Credit ITV