poatel Africa
Friday, 16 January 2015
0 No comments
Andressa Urach alimaliza wa pili
katika mashindano ya urembo ambapo mashabiki walimpigia mwanamke
waliyehisi kuwa na makalio mazuri zaidi katika nchi yao kupitia kwenye
mtandao wa internet.
Ili kujiongeza urembo, Urach aliambia jarida
la Daily Mail la Uingereza kwamba alidungwa sindano za kemikali ili
kufanya makalio yake kuwa makubwa pamoja na kuongeza ukubwa wa miguu
yake.
Lakini mnamo mwaka 2013, mwili wake ulianza kuoza ndani.
Athari
za kujiweka urembo bandia zilianza kumwandama wakati Urachhadi
madaktari wakalazimika kutoa kemikali hizo kutoka mwilini mwake mwezi
Novemba kwa kuchimba mashimo katika mapaja yake.
Mwili wake ilipatwa na mshtuko kwa sababu ya ugonjwa alioupata kwa kutumia vifaa chafu vya matibabu mwilini mwake.Madaktari wametoa kemikali za sumu mwilini mwa Urach
Daktari mmoja wa kurekebisha na
kutibu athari zinazotokana na urembo bandia alisema ugonjwa aliopuata
Urach ulitokana vifaa chafu.
Madaktari hata hivyo waliweza kuokoa
maisha yake lakini hadi leo anatumia tu kiti cha magurudumu na miguu
yake ina mashimo mwengi ambayo madaktari waliweza kutoboa ili kutoa
kemikali zenye sumu alizotumia kuongeza ukubwa wa makalio na miguu.
''Ninalipia
makosa yangu leo kwa sababu nilitaka urembo kwa kila hali, ili
nionekane kuwa kamili. Mungu ananiadhibu'' Urach aliambia Mail.
''Lakini badala ya kujiongeza urembo, niliharibu mwili wangu na sasa hata hauna sura.'' Urach anasema Mungu alimpiga kiboko kwa kujaribu
kujibadilisha mwili wake kwa sababu ya kujitakia umaarufu
Urach pia alisema kwamba
alikuwa na mazoea mabaya ya kufanyiwa uapasuaji wa kujiongeza urembo
bandia kila alipojihisi kufanya hivyo.
''Sikuwahi kutafakari mara
mbili wakati nilipokuwa nafanyiwa upasuaji lakini watu waliponionya
nilidhani tu nitaweza kukabiliana na athari za hayo baadaye. ''
Ningeweza kwenda kwa daktari, kama mfano nilivyozoea kwenda dukani na
kuchagua nilichokitaka. Nilitaka watu wanitazame na kusema tu , ''wow''
Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.