Bohari
ya Dawa nchini Tanzania, MSD imeripotiwa kuwa imesitisha utoaji wa dawa
muhimu kwa taasisi za afya za serikali hadi hapo deni la shilingi
bilioni 90 linalodaiwa na wakala huyo litakapolipwa na taasisi hizo.
Sikika
ambalo ni shirika lisilo la kiserikali linalohimiza huduma bora za afya
nchini Tanzania limeeleza Jumapili kwamba kiasi kikubwa cha fedha
kinachodaiwa na MSD kime mamlaka hiyo ya usambazaji dawa kushindwa
kununua dawa kwa ajili ya zahanati, vituo vya afya na taasisi nyingine
za tiba nchini kote.Hivi karibuni MSD ilisema miongoni mwa taasisi za tiba zinazodaiwa na wakala huyo ni pamoja na Hospitali ya Taifa Muhimbili kiasi cha shilingi bilioni 8 hali ambayo imesababisha MSD kusita kuendelea kununua dawa muhimu kwa ajili ya hopsitali hiyo zikiwemo dawa za kutibu wagonjwa wa figo.