1. Awamu ya pili kwa
vijana watakaojiunga na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mujibu wa Sheria
itaanza rasmi tarehe 11 septemba, 2014 na itahusisha makundi yafuatayo:-
- Walimu wote ngazi ya cheti (GATCE) 2014 ( Waliomaliza mwaka 2014).
- Walimu elfu tatu (3,000) ngazi ya Diploma (DSEE) (Waliomaliza mwaka 2014).
- Vijana waliomaliza kidato cha sita mwaka 2014 waliopangwa awamu ya pili ambao hawana sifa za kujiunga na vyuo vya elimu ya juu (Vyuo Vikuu).
2 . Vijana
waliomaliza kidato cha sita mwaka 2014 ambao walipangwa kujiunga na JKT
awamu ya pili na wana sifa za kujiunga na elimu ya vyuo vya juu (Vyuo
Vikuu) wanatakiwa kuandika barua ya kuahirisha kuhudhuria mafunzo ya JKT
mpaka hapo watakapomaliza masomo yao. Barua hizo ziwe zimefika Makao
Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa kabla ya tarehe 15 Agosti, 2014.
Barua zinaweza kutumwa kwa:-
- Anwani
- Mkuu wa JKT
- Makao Makuu ya JKT
- P.o.Box 1694, Dar es Salaam
- E-mail: info@jkt.go.tz (barua iwe na sahihi ya mhusika na ifanyiwe “scanning”).
- Barua iletwe na mhusika Makao Makuu ya JKT.
3. Awamu ya tatu ambayo itahusisha walimu wa Diploma (DSEE) itaanza mwezi Januari 2015.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA