Mwanamke huyo baada ya kujifungua akiwa amezungukwa na watu waliokuwa wanamhudumia.
Watu wa huduma za afya wakiwa wamemzungushia mashuka ‘mzazi’ huyo.
Magari ya huduma yakiwa yamefika kumchukua mama na mwanawe katika duka la Primark.
MWANAMKE mmoja ambaye jina lake halikuweza kujulikana mara moja,
aliwashangaza wapita njia katika jiji la Birmingham, Uingereza, majuzi
baada ya kujifungua mtaani nje ya dula na nguo la Primark.
Mama huyo alijifungua salama-salmin mtoto wa kike baada ya kuzidiwa
uchungu akiwa kando ya barabara. Wapita njia waliokuwa wakipita mtaani
majira ya saa nane alasiri walimtafutia gari la wagonjwa, wakamwekea
mablanketi chini na kumzungushia mashuka mama huyo ambaye alikuwa
amelala chini ili kumsitiri.
Watu wengi walifikiri kulikuwa na onyesho fulani mtaani hapo, lakini
wakagundua ni mama huyo alikuwa amejifungua. Mama na mtoto walipelekwa
Birmingham City Hospital kwa huduma zaidi.