Mwanamuziki zao la nyumba ya kukuza vipaji Tanzania ‘THT’, Amini Mwinyimkuu.
Mwanamuziki zao la nyumba ya kukuza vipaji Tanzania
‘THT’, Amini Mwinyimkuu amefunguka kuwa, aliamua kufunga ndoa ya fasta
ili kuuwahi mwezi mtukufu wa Ramadhani.“Ni kweli nilioa juzi pale Magomeni Mwembechai, ilikuwa ni ndoa tu na niliamua kufanya hivyo ili kuuwahi mwezi Mtukufu wa Ramadhani,” alisema Amini ambaye ndoa ilimbadili jina kwa kufungishwa kwa jina la Namini kufuata mambo ya kinyota.