Baraza
la mitihani Tanzania NECTA limetangaza rasmi matokeo ya Kidato cha Nne
2012. Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka
jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la
Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya
ufaulu.
Matokeo
hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la
nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali
na huenda yakafikia asilimia 57.
Kwa matokeo hayo, watahiniwa
wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao
watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani
huo walifaulu.
Matokeo ya awali
yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru
Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani
wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza
mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la
nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia 28.1.
Katika matokeo hayo,
watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu ambayo
imebadilika katika matokeo mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata
daraja hilo ni 158,100 ambayo ni asilimia 43.
KUPATA MATOKEO MAPYA YA KIDATO CHA NNE 2012>>BOFYA HAPA<<