Header ads

Header ads
» » Mfahamu James Goodfellow, mgunduzi wa mashine ya kutolea Pesa ATM


Kama wewe ni mtumiaji wa ATM usisahau kutoa shukrani zako za dhati kwa mgunduzi wa mashine hizo za kutolea pesa duniani kila unapoenda kutoa pesa.
Katika miaka ya 1960, Goodfellow alikuwa akifanya kazi kama muhandisi katika mashirika ya Glasgow, ikiwa ni sehemu ya kiwanda cha Smiths alipewa kazi maalumu ya kusadia wateja wanaochelewa benki siku za wikiendi hasa pale benki zinapofungwa. Kwa mujibu wa Goodfellow watu wengi walikuwa wakikosa huduma za kibenki kwa sababu walikuwa wakikosa muda siku za katikati ya juma na siku za wikiendi benki zilikuwa zikifungwa mapema.

Baada ya kufikiria kwa makini akaona mashine ndio suluhisho la tatizo hili, akaja na mashine ya kutoa pesa ikihusisha PIN (Personal Identification Number) kama utambulisho wa muhusika wa akaunti. Serikali ya Uingereza ikampa hati miliki ya kuwa mgunduzi wa PIN.
 James Goodfellow, ATM Machine
Goodfellow alitengeneza kadi ya plastiki yenye matundu ambayo ilikuwa ikipachikwa kwenye mashine ya kutoa fedha kabla ya mtumiaji kutakiwa kuingiza tarakimu 10 zikiwa pamoja na PIN zake ili kuweza kutoa fedha, kwa sasa zinafahamika kama ATM cards.
Baada ya Goodfellow kutengeneza mashine ya mfano, ruhusa ilitolewa na matawi ya benki za Westminster Bank zikawa benki za kwanza kutumia mashine hizo mnamo mwaka 1967.

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post