Header ads

Header ads
» » Huawei yaandaa maonyesho ya vifaa na huduma za kiteknolojia nchini Zambia

 ZAMBIA-LUSAKA-CHINA-HUAWEI
Kampuni kubwa ya vifaa vya elekroniki ya Huawei kutoka China, imeandaa maonyesho ya kiteknolojia siku ya Jumatano nchini Zambia.
Katika maonyesho hayo, Huawei ilitambulisha vifaa vya mawasiliano pamoja na huduma za teknolojia ya kisasa.
Kampuni ya Huawei ilitoa maelezo na kuarifu kwamba lengo lake ni kusaidia kurahisisha mawasiliano na shughuli za kikazi za serikali na taasisi za umma nchini Zambia kwa kutoa vifaa na huduma bora.
Waziri wa uchukuzi na mawasiliano wa Zambia pamoja na balozi wa China nchini humo walihudhuria kwenye maonyesho hayo.
Kampuni ya Huawei imekuwa ikiendesha shughuli zake za kibiashara nchini Zambia kwa kipindi cha miaka 12.
Chanzo:  xinhuanet.com

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post