Header ads

Header ads
» » Mwalimu na Mwanafunzi Nchini Korea watengeneza betri ya smartphone inayokaa na chaji kwa Wiki moja


Teknolojia mpya ya utengenezaji betri iliyotengenezwa na mwalimu na mwanafunzi wake wa PhD huko nchini Korea Kusini itawezesha kifaa kama simu kukaa na chaji kwa wiki moja nzima bila kuchaji. Profesa Choi na mwanafunzi wake wa chuo kikuu cha Pohang wametengeneza betri la aina ya ‘solid oxide’ {solid oxide fuel cell (SOFC)} wakiwa na lengo la betri hilo kutumika badala ya betri za sasa hivi ambazo ni za ‘lithium-ion’.
 Creators.JPG

    Prof. Choi & Mwanafunzi wake  Kun Joong Kim​

Betri zinazotumika katika simu, tableti, drone na vifaa mbalimbali vya elektroniki kwa sasa ni za teknolojia ya Lithium-ion. Betri hizi zinakiwango kidogo za uhifadhi wa chaji. Teknolojia hii iliyogunduliwa na Profesa Choi na mwanafunzi wake, Bwana Kun Joong Kim imepokelewa vizuri kwani inaweza kutumika ata kwa betri kubwa kama zile zinazoitajika kwenye magari yanayotumia umeme.
Creating SOFC. 
Utengenezaji wa SOFC kutumia TLC
Teknolojia hii inategemea utumiaji wa Hydrogen, ikiwa pia na sifa ya utengenezaji usio mgumu sana huku ‘electrolyte’ zake zikiwa na sifa kubwa ya kutopotea kwa urahisi – hivyo uwezo wa kukaa na chaji kwa muda mrefu. Kwa teknolojia hii vifaa kama simu janja zitaweza kuchajiwa mara moja tuu kwa wiki huku vifaa kama vile drones vitaweza kutumika kwa zaidi ya lisaa limoja. Hii ni tofauti na sasa ambapo simu nyingi huchajiwa kila siku huku drone zikiweza kurushwa chini ya lisaa limoja kabla ya kuitaji kuchajiwa.
 Fahamu zaidi Project
CHANZO; postech.ac.kr
MHARIRI; Abdallahmagana.com

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post