Header ads

Header ads
» » » Njia rahisi ya Kurudisha Mafaili yaliyofutika kwenye Kompyuta au Simu


Ikiwa kwa makusudi au hata bahati mbaya umefuta data zako katika memori kadi ya simu yako, ‘hard drive’ au kifaa kingine, na baadae ukawa unazitaka tena, je unaweza zipata? Ndio unaweza zipata!. Unaweza pata tena data zako ulizofuta katika SD Card / Hard Disk Drive kwa msaada wa Asoftech software. Asoftech ni programu ya kuzifufua data zilizofutwa ambayo ni ya bure ku-download na rahisi kutumia na pia ina ukubwa mdogo (kama 4MB hivi) kwa msaada wa hii programu (software) utafufua mafaili yaliyofutwa kwenye vifaa vya uhifadhi wa data mbalimbali kama vile ‘pen drive, USB drive, external Hard Drive, memory card’ na sehemu zingine. Inabidi kuacha kutumia mafaili katika simu yako mara tuu unapotaka kurejesha mafaili yaliyofutika katika SD Card kwa sababu haitawezekana kurejesha mafaili wakati mafaili mengine yanatumika muda huohuo katika simu. Kitu kingine cha kuweka akilini ni kwamba hautawezekana kufufua mafaili kwa kutumia Asoftech kama utakua umefomati (Format) SD Card/Hard Drive ya kifaa chako. 

FUATA NJIA ZIFUATAZO KUREJESHA  MAFAILI YALIYOPOTEA

1. Kwanza kabisa inabidi Kupakua (download) programu (Software) ya Asoftech
 Card Data Recovery
2. Baada ya kupakua (download) fanya mpango wa kuifadhi (install) itakuchukua muda kidogo tuu  3. Kutumia Asoftech inakubidi uwe ‘Administrator’ katika kompyuta yako, kama ni Admin nenda mpaka kwenye icon ya Asoftech ‘ Right Click’ kisha bofya ‘ Run As Administrator ‘. 

 4. Baada ya hapo unganisha simu yako au kifaa kingine katika kompyuta yako. Hakikisha kompyuta yako inasoma memori kadi ya simu yako. Au kama unaweza toa memori kadi ya simu weka katika sehemu ya kusoma kadi (card reader)na uunganishe katika kompyuta. Kama unataka fufua mafaili katika Hard Disk Drive ya kompyuta yako unaweza ruka hatua hii. 

5. CHAGUA Diski Uhifadhi (DRIVE) 
 SD Card File Recovery Software
Chagua Drive Hatua ya hapo juu ikipita na Asoftech ikifunguka zitatoka orodha ya diski uhifadhi kibao, chagua moja ambayo unataka kufufua data zake. Chagua drive ya Sd card au Hard drive nyingine na kisha bofya NEXT 

6. Itaanza fanya uchambuzi katika diski/ SD card yoyote uliyoichagua. Uchambuzi ukishakamilika itatoa orodha ya mafaili mengine na maelezo ya aina zake (kama vile mp3 au .jpg na zingine) 
7. FUFUA MAFAILI 
 SD Card Recovery Software
 Fufua Mafaili Sasa unaweza kubonyeza “recover’ kufufua mafaili uliyo yachagua na pia unaweza kutochagua mafaili ambayo hutaki kuyafufua. 

Kwa kutumia njia hii unaweza fufua aina yoyote ya faili katika Hard Disk Drive na hata SD card

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post