Header ads

Header ads
» » » Burundi imepiga marufuku umiliki wa laini za simu zaidi ya moja


 Idhaa moja ya redio ya Bonesha FM imeripoti kuwa imepata taarifa hiyo kutoka kwa wizara ya fedha
Kampuni zinazotoa huduma za mawasiliano ya simu zimepewa kipindi cha miezi miwili kutekeleza sheria hiyo mpya.
Kampuni hizo zitalazimika kusajili wamiliki wote wa laini za simu la sivyo wataadhibiwa na faini ya takriban dola $3,000 kwa kila laini ambayo itatumiwa pasi na kusajiliwa.
Sheria hii mpya imewekwa baada kutokea machafuko ya kisasa kwa takriban mwaka mooja sasa
Machafuko nchini humo yalianza mwezi Aprili mwaka uliopita baada ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania muhula wa tatu.
Wapinzani wake wanasema kuwa hatua hiyo ya Nkurunziza inakiuka katiba ya taifa inayomzuia rais kuongoza kwa zaidi ya miaka 10 ama mihula miwili.
Nigeria iliiadhibu kampuni ya mawasiliano ya MTN faini ya dola bilioni 5.2 kwa kuendelea kuruhusu utumizi wa simu ambazo hazijasajiliwa.
 
MTN-Nigeria Map
Rais Muhammadu Buhari aliilaumu MTN kwa kuruhusu wapiganaji wa Boko Haram kutekeleza mashambulizi nchini 
humo kwa kuruhusu laini za simu ambazo hazijasajiliwa 
kuendelea kutumika hata baada ya ilani ya kutofanya hivyo.

CHANZO: BBC NEWS
MHARIRI: Abdallahmagana,com

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post