Header ads

Header ads
» » Waziri wa Ulinzi wa Hungary ajiuzulu wazifa huo

 Waziri wa Ulinzi wa Hungary ajiuzulu

Csaba Hende awasilisha barua ya kuijuzulu kama Waziri wa Ulinzi wa Hungary

Waziri wa Ulinzi wa Hungary Csaba Hende, ameripotiwa kuwasilisha barua ya kujiuzulu siku ya Jumatatu, iliyopokewa na kukubaliwa na Waziri Mkuu wa nchi Viktor Orban.
Baada ya uamuzi huo, Orban alimpa Istvan Simicsko mamlaka ya kuongoza Wizara ya Ulinzi.
Simicsko alikuwa akihudumu kama katibu mkuu wa Wizara ya Rasilimali tangu mwaka 2014.
Kwa mujibu wa maelezo ya ofisi ya habari za serikali, inaarifiwa kwamba kabla ya Hende kuwasilisha barua ya kujiuzulu, baraza la usalama la kitaifa lilikuwa limekutana kwa ajili ya kujadili suala la uhamiaji na kupokea ripoti ya ujenzi wa uzio wa kilomita 175 mpakani mwa Hungary na Serbia.
Hende ambaye amekuwa akihudumu kama Waziri wa Ulinzi tangu mwaka 2010, aliwasilisha barua ya kujiuzulu baada ya mkutano huo.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post