Utawala wa kifalme nchini Swaziland
unaongozwa na mfalme Mswati umetakiwa kufutilia mbali sherehe maarufu za
kitamaduni baada ya wasichana kadha waliokuwa wakisafiri kwenda kwa
sherehe hizo kufa kwenye ajali ya barabarani.
Kundi linalounga
mkono demokrasia nchini humo la (the Swaziland Solidarity Network)
limetoa wito kwa mfalme Mswati kufutilia mbali sherehe hizo ambazo
wasicha walio nusu uchi hucheza mbele ya mfalme.Kundi hilo linasema kuwa zaidi ya wasichana 60 waliangamia wakati lori walilokuwa wakisafiria lilihusika kwenye ajali ya barabarani.
Utawala nchini Swaziland unasema kuwa idadi ya wasichana waliokufa ni 13.