Mwenyekiti wa Wamiliki wa vyombo vya Habari nchini – MOAT Dr Reginald Mengi ametoa tahadhari hiyo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa Mashauriano ya Amani na Utulivu nchini, na kusisitiza kuwa kupitishwa kwa miswada hiyo kutasababisha ukiukwaji mkubwa wa Uhuru wa Habari, uvunjifu wa amani, na ni kifo kwa vyombo vya habari binafsi nchini.
Akitolea mfano, Dr Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP amesema kifungu nambari 14 cha muswada wa sheria ya Huduma za Vyombo vya habari kinatoa amri kwa vituo binafsi vya Utangazaji kujiunga na chombo cha habari cha umma kwa ajili ya Taarifa ya habari ya kila siku saa mbili usiku, kinyume na ilivyo sasa, na ni dalili za kurudi tulikotoka.