Header ads

Header ads
» » Wakati Tanzania Ikijianda na Uchaguzi,Bila Kujua Hatima ya Katiba Mpya: Maandamano yazuka Nchini Burundi Kupinga Uchaguzi wa Urais

 
Kumezuka ghasia katika mji wa Bujumbura nchini Burundi kati ya maafisa wa polisi na waandamanaji wanaoishtumu serikali kwa kufanya mapinduzi ya kikatiba.
Waandamanaji walirusha mawe na kuchoma matairi huku maafisa wa polisi wakilazimika kurusha vitoa machozi na risasi bandia hewani.
Ghasia hizo zinafuatia tangazo siku ya jumamosi kwamba rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameteuliwa na chama chake kuwania muhula wa tatu wa urais.
Upinzani umeitaja hatua hiyo kama ukiukaji wa katiba,na kuonya kuwa huenda ikaathiri makubuliano ya amani ambayo yalimaliza miaka kadhaa ya mapigano ya kikabila.
Serikali imesema kuwa maandamano hayo si halali.
Maelfu ya raia wa Burundi wamelitoroka taifa hilo katika majuma ya hivi karibuni wakihofia kuongezeka kwa ghasia hizo huku taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi mnamo mwezi Juni.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post