Header ads

Header ads
» » Ukosefu wa Ajira chanzo cha Uhalifu

Need-Work
Ukosefu wa Ajira unachangia kwa Asilimia kubwa, ongezeko la Wimbi la Uhalifu Duniani na kusababisha Machafuko makubwa na uhalifu huu usababishwa na Vijana wanao hitimu masomo yao,  kwa kutumia taruma zao kufanya uharifu huo, kuakikisha maisha yao yanakwenda vizuri
Kwa mfano sasa kumeibuka Wizi wa kila aina kama wizi wa fedha kwa njia ya mtandao kupitia mashine maalum za kutolea fedha (ATM) unaendelea kuzitesa benki mbalimbali nchini ambapo kwa sasa wahalifu hao wanahamisha fedha za wateja wakiwa nje ya nchi kwa kutumia kadi za kutolea fedha.

Wizi huo hufanyika kwa kutumia kadi za kutolea fedha zinazoingiliana na benki zingine (smart card) ambazo mteja wa benki anaweza kutolea fedha akiwa popote duniani kupitia ATM.


Wizi huu ufanywa na Wasomi wenye Taaluma zao, Waliokaa mitaani pasi na Ajira na kuamua kufanya wizi huu
 Afisa mmoja wa benki ambaye hata hivyo, hakupenda jina lake litajwe  na kukiri kuwa kuna wizi wa fedha wa mara kwa mara kwa njia ya mtandao ambao benki umeshaugundua.

Alisema wezi hao hutumia njia mbali mbali kujua password za watu ikiwemo ya kuweka kamera ndogo kwenye ATM na vile vile kwa kutumia utalaam wa kiteknolojia wa hali ya juu kusoma taarifa za benki na kuzitumia kuiba fedha kwenye akaunti za watu.

Alishauri wanaopenda kutoa fedha kwenye ATM waende kwenye ATM zilizo kwenye matawi ya benki husika kwa kuwa wanaoweka kamera sio rahisi kwenda kwenye matawi ya benki.

Aidha, aliwataka wateja kuwa na utaratibu wa kuangalia akaunti zao mara kwa mara ili kubaini kama kuna tofauti yoyote kwenye fedha zao.
NIPASHE ilipotaka kauli ya Waziri wa Fedha kuhusu wizi huo, simu yake haikuwa na majibu.

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilishawahi kukaririwa kuwa itaendelea kufanya utafiti wa kuwabana wezi hao.

Kauli hiyo ilitolewa na Gavana wa benki hiyo, Profesa Benno Ndulu, wakati akizungumzia wizi wa mitandao na kuongeza kuwa licha wa wizi huo kufanyika, huduma za kibenki zitaendelea kutolewa kwa kuwa ni mkombozi wa wateja.

Aidha, alisema wameziagiza benki kuweka kifaa cha umeme (electronic chip) kwenye kadi zao za ATM ambazo si rahisi kughushi.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post