Mrembo wa Afrika Kusini Rolene Strauss ameshinda Miss World 2014 nakuchukuta taji kutoka kwa Megan kutoka Philippines kwenye show iliyofanyika ExCeL Exhibition Centre mjini London.
Rolene mwenye miaka 22 ambaye ni mwanafunzi anayesomea udaktari alisema “Hii kwaajili ya Afrika Kusini, nitajipanga kwaajili ya kinachokuja kutokea, haya ni majukumu makubwa sana ”
Megan naye alisema ” Natarajia Rolene atakuwa na furaha kwenye mwaka wake kama mimi ”
Mshindi wa pili ni Edina Kulcsar wa Hungary na watatu ni kutoka Marekani Elizabeth Safrit.