Header ads

Header ads
» » GOOGLE WAMUENZI WANGARI MAATHAI,MWANAMKE KUTOKA KENYA KATIKA HOMEPAGE YAO




Wangari Muta Maathai: Mapigano ya Mwanamke Mmoja Kuwapa Sauti Wanaoikosa


Wangari Muta Maathai ni mtu muhimu sana katika historia na maendeleo ya Afrika ya Mashariki. Maathai ni mwanmke ambaye amekuwa wa kwanza katika mambo mengi. Alipata shahada ya uzamifu ya kwanza iliyotolewa kwa mwanmke wa Afrika ya Mashariki. Maathai pia alikuwa mwanamke wa kwanza kushikilia vyeo vya mwenyekiti na mwalimu mkuu katika chuo kikuu cha Afrika ya Mashariki. Mwisho, Maathai alikuwa mwanmke Mwafrika wa kwanza kuipokea tuzo ya Nobel. Amefanya kazi ngumu kuvipata vitu vikubwa na kuviunda vitu vikubwa. Wangari Maathai ni mfano mzuri kwa wanawake wote ulimwenguni, hasa katika Afrika ya Mashariki. Hadithi yake inafuata.

Malezi na Elimu

Wangari Maathai alizaliwa tarehe moja, mwezi wa nne, elfu moja mia tisa na arobaini. Anatoka kabila la Kikuyu. Wazazi wake walipata maisha kama wenyeshamba katika ardhi juu karibu Mlima Kenya. Maathai alizaliwa na kulia kata ya Nyeri katika Kenya. Baada ya kumaliza shule ya msingi, Maathai alienda Limuru kuendelea na masomo katika Shule ya Sekondari ya Loreto Convent.
    Baada ya kuhitimu shule ya sekondari, Maathai alikuwa mmoja wa wanawake wachache kuongeza elimu ya juu. Alienda Marekani kusoma Biolojia. Shahada ya kwanza alipata mwaka wa 1964 katika Mount St. Scholastica, chuo kikuu kidogo katika jimbo la Kansas. Maathai aliendelea na masomo kupata shahada ya pili katika masomo ya Biolojia Chuoni Pittsburgh. Ameshafika hadhi ambayo wanawake wachache wa Afrika walikuwa wamediriki kuifikia, lakini Maathai hakusimama hapo. Alirudi nchini kwake Kenya aliposoma tena Chuoni Nairobi  kupata shahada ya uzamifu. Ingawa aliolewa kwa mashaka na hata kukumbana na mkingamo kutoka kwa wanafunzi na walimu wa kuume, Maathai alipanda cheo. Katika 1971, alikuwa mwanmke wa kwanza kupata shahada ya uzamifu, aliyopata katika Anatomia ya Wanyama. Mara moja alianza kufundisha masomo hayo katika chuo kikuu cha Nairobi.

Maswali

1. Wangari Maathai alikulia katika mazingira ya aina gani?
2. Maathai alisoma masomo yapi?
3. Kama mwanamke, mafanikio makuu ya Wangari katika elimu yalikuwa yapi?


Maisha katika Taaluma ya Elimu na Maisha ya Kibinafsi

Uingiaji wa Maathai katika taaluma ya elimu ulifikiwa na fanaka, na alipanda vyeo. Katika 1976, miaka mitano tu baada ya kuanza kufundisha katika chuo kikuu, Maathai aliteuliwa Mwenyekiti wa Idara ya Anatomia ya Wanyama. Mwaka uliofuata alikuwa profesa mshiriki. Alikuwa mwanmke Mkenya wa kwanza kufikia vyeo vyote viwili. Wakati wa muda huu wa shughuli chuoni, pia Maathai alikuwa na matukio mengi katika maisha yake ya kibinafsi. Wangari aliolewa na mwanasiasa Mwangi Mathai mwaka wa 1969. Walikuwa hawajaona hata kwa miaka kumi na mitano mume wa Wangari alipoomba kumwacha. Mwangi Mathai alidai kwamba mke wake alikuwa ngumu mno kufaa kama mke mzuri kwa sababu hakuweza kumtawala. Hakimu aliyekuwa anaamua kesi hii aliafikiana na Mwangi na aliidhini talaka. Wangari alijaribu kutoa mawazo bila kusita kupinga hakimu na alirushwa kizuizini. Hakimu pia alimwagiza Wangari aache kutumia jina la mume wake. Ili Wangari adhihirishe uaminifu na uasi wake, aliweka herufi nyingine ya “a” tu.


Maswali

1. Maathai alifanikiwaje katika taaluma ya elimu?
2.  Kwa nini mume wake alitaka kumtaliki Wangari?
3.  Je, Wangari alijibu uamuzi wa hakimu kulibadilisha jina lake?


Maisha ya Siasa ya Maathai

Wangari Maathai anafahamika vizuri kwa kupiga vita ufisadi wa kisiasa. Alitoa mawazo bila kusita wakati wa amri ya serikali ya Rais Moi. Maathai alikuwa na mahasimu wengi katika serikali hii kwa sababu aliikosoa kwa kuongoza katika ufisadi na siasa za kikabila. Licha ya mashitaka haya, alianzisha harakati za kudai chaguzi za vyama vingi. Maathai alishambuliwa na kurushwa kizuizini mara kadhaa wakati huu. Maathai pia alihusika na shughuli za serikali katika mazingira. Mwaka wa 1989, Maathai, peke yake, alizuia ujenzi wa ghorofa katika bustani ya Uhuru Park katika mji wa Nairobi. Ghorofa ilikuwa inapangwa kujengwa na Kenya Times Media Trust, washarika wa biashara wa Rais Moi. Alipopewa Tuzo la Uongozi wa Afrika katika 1991 na Umoja wa Mataifa Maathai alisema:

    Si kwamba viongozi hawaelewi athari mbovu za mifumo isiyohaki ya  kisiasa na kiuchumi inayoendeleza uharibifu wa mazingira na maendeleo yasiyo endelevu. Biashara hii, itakataliwa lini na jumuia ya ulimwengu? ....Changamoto za Afrika zinakabiliwa katika viwango vingi, na kuna fanaka ndogo ambayo imepatikana lakini kwa kasi ndogo sana. Dhana za maendeleo endelevu, vielelezo mwafaka vya maendeleo mazuri, na maendeleo yanayojumuisha wengi si za kigeni. Sisi tunajua kwamba watoto wetu na vizazi vijavyo vina haki ya kuishi katika dunia ambayo pia itahitaji nishati, isiyokuwa na uchafuzi wa mazingira,  tajiri kwa kuwa na wingi wa viumbe mbalimbali, na yenye hali ya hewa inayoruhusu aina zote za maisha. (1)

Labda Maathai aliona kwamba maendeleo katika siasa yalikuja polepole mno akipofanya kazi nje. Kuyabadilisha mambo ya siasa, mara nyingi unahitaji kuanza kutoka ndani ya kiini cha tatizo. Katika mwaka wa 1997, Maathai aliingia katika uchaguzi wa urais wa Kenya. Lakini kabla ya uchaguzi chama chake kilimdondosha kama mgombea wake katika uchaguzi. Maathai pia alishindwa katika uchaguzi wa ubunge.
    Mwaka wa 2002, ulileta mabadiliko mengi. Chama cha Kenya African National Union kilishindwa na National Rainbow Coalition uchaguzini. Maathai pia alichagulika bungeni. Serikali chini ya Rais Mwai Kibaki iliafikiana zaidi na Maathai. Kutoka 2003 mpaka 2005, alihudumu kama waziri msaidizi wa Mazingira, Mali Asili, na Wanyama. Shughuli zingine za siasa za Maathai ni zinazofuata zikiwemo: katika 2003 alikianzisha Chama cha Mazingira Green Party cha Kenya, na 2008 atakuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa utakaoleta pamoja watu wa vyama vya kijani kutoka ulimwenguni kote. Maathai pia alichaguliwa kuwa Rais wa kwanza wa Baraza la Uchumi, Jamii, na Utamaduni la Umoja wa Afrika.

Maswali
1.  Kwa sababu gani Maathai hakuafikiana na serikali ya Rais Moi?
2.  Maathai alishikilia vyeo vipi katika serikali ya National Rainbow Coalition?


Mazingira na Uhamasishaji wa Wanawake   
Wangari Maathai ni mwanasiasa muhimu wa Kenya, lakini watu wanamfahamu zaidi kwa kazi yake katika sehemu za mazingira na maendeleo ya wanawake. Kuanzia 1976 mpaka 1987, Maathai alifanya kazi na Maendeleo Ya Wanawake katika Kenya. Ilikuwa hapa alipofikiri kwa mara ya kwanza dhana ya kufundisha wanawake kufanya mipango ya kupanda miti. Dhana hii ilimuongoza kuanzisha shirika la Green Belt katika 1977.
Green Belt Movement ni shirika lisilo la kiserikali. Maathai aliona kwamba wanawake wengi wa Afrika ya Mashariki walikosa njia nzuri ya kupata pesa kujitetea na kuwatetea wenzao. Maathai aliamini kwamba kupata mahali pa kudumu uchumini, wanawake wangehitaji kushiriki katika shughuli ambazo zilikuwa endelevu kimazingira. Kwa hivyo, Maathai alipoanzisha Green Belt Movement alikuwa na malengo mawili: kwamba shughuli ambazo zingefundishwa zingewasaidia wanawake kupata hela na kuboresha hali yao ya maisha, na pia kwamba zingekinga mazingira. Shirika hili linawafundisha wanawake namna ya kufanya kazi mbalimbali kama kupanda miti, kulinda mizinga ya nyuki, na kutengeneza vyakula. Tangu kuanzishwa kwa Green Belt Movement, miti milioni 30 imepandwa mashambani mwa wanawake, na pia mashuleni na makanisani. Maathai alitoa hotuba katika chuo kikuu cha Harvard akasema: “wanawake wa Green Belt Movement wamejifunza kuhusu vyanzo na dalili za uharibifu wa mazingira. Wameanza kuelewa kwamba ni lazima wao, na siyo serikali yao, wawe walinzi wa mazingira” (1). Kwa sababu ya kazi yake yote na Green Belt Movement, Maathai alipatiwa jina la “mwanmke wa mti.”

Swali
1. Alipoanzisha shirika la Green Belt Movement, Maathai alitaka kufanikisha nini?


Shughuli na Vyeo Vingine

Licha ya wajibu wake mkubwa wa kufundisha, kufanya kazi serikalini, na kuongoza Green Belt Movement, Maathai pia alikuwa amehusika katika shughuli zingine mbalimbali. Kwa mfano, katika 1998, Maathai alijunga na Jubilee 2000 Coalition alipotetea ufutaji wa madeni ya mikopo kwa nchi maskini za Afrika. Pia alifanya kampeni kupinga wizi wa ardhi za pori za umma. Katika 2002, Maathai alikikubali cheo cha msomi mgeni (Visiting Fellow) Chuoni Yale. Aliibeba bendera katika sherehe ya kwanza ya Michezo ya Olimpiki ya 2006. Maathai pia ni mwandishi. Ameshavichapisha vitabu viwili vinavyoitwa: The Green Belt Movement: Sharing the Approach and the Experience; na Unbowed: A Memoir.

Tuzo ya Nobel ya Amani

Katika mwaka wa 2004, Wangari Maathai alikuwa mwanmke Mwafrika wa kwanza kuipokea Tuzo ya Nobel ya Amani. Maathai alituzwa kwa sababu zinazofuata: msaada wake katika maendeleo endelevu, demokrasia, na amani; kwa kusimama kama shujaa kupinga serikali dhalimu ya awali ya Kenya; kwa sababu matendo yake yamesaidia kuangaza macho kwa udhalimu wa kisiasa katika Kenya na ulimwenguni kote; na kwa kuwa mfano mzuri kwa watu wengi mapambanoni mwa haki za kidemokrasia na hasa ametia moyo wanawake kuboresha hali zao.

Maswali
1.  Maathai alifanya nini alipofanya kazi na Jubilee 2000 Coalition?
2.  Kwa sababu zipi Maathai alipatiwa Tuzo ya Nobel?


Shutuma
Ingawa sasa ni vigumu kupata  ukosoaji wazi kuhusu Wangari Maathai (hasa baada ya kupokea Tuzo ya Nobel), kuna uvumi ambao unadokeza mambo yasiyo mazuri kumhusu. Kwanza, Maathai alikuwa amekosolewa kwa kuitetea imani kwamba Virusi Vya Ukimwi vilitengenezwa na wanasayansi maabarani katika nchi za Kimagharibi na vilifunguliwa katika Afrika ili kuwaharibu watu Wafrika. Maathai amesema kwamba uvumi huo si kweli. Ametoa maelezo na kusema: “nimewatahadharisha watu kupinga taarifa mbaya kuhusu kiini cha VVU....maoni haya ni mabovu na ya huharibu” (4). Kuna shutuma nyingine, lakini, ambayo haijaongelewa mno. Maathai amekosolewa kwa kitu kimoja ambacho hudai kukipiga vita na kukipinga: ufisadi na kutokuwa mwaminifu. Watu wamesema kwamba pesa zilizotolewa kwa Green Belt Movement hazikutumiwa kufanya vitu zilivyopaswa. Wamesema kwamba pesa nyingi hazikuonwa na wanawake vijijini.
Ni vigumu kujua nini ni kweli na nini si kweli. Wangari Maathai amefanya maendeleo mno kwa Waafrika, kwa wanawake, na kwa mazingira, natumaini hayataharibika kwa sababu ya udhaifu wa binadamu na mlungula.


Maswali

1.  Ni vipi Wangari Maathai amekuwa wa kwanza katika mambo mengi?

2.  Je, unafikiri maathai ni mfano mzuri kwa wanawake wa Afrika?

3.  Kwa maoni yako, ni bora kujaribu kufanya kazi kwa vyanzo vingi ama kumakinikia kabisa katika kitu kimoja tu?

4. Unaamini mashtaka na uvumi kuhusu Maathai ni kweli? Kwa maoni yako, mashtaka hayo yanapasa kubakia kama siri?

5. Kutokana na vitu vyote vingine vizuri ambavyo amefanya Maathai (kwa mazingira, kwa wanawake, na kupigana ufisadi wa siasa) ni bora kumsamehe kwa uongozi mbaya katika shirika la Green Belt Movement?

Marejeleo

1.    “About Wangari Maathai.” The Green Belt Movement. 20 May, 2007. http://greenbeltmovement.org/w.php?id=3.

2.    “Wangari Maathai” About.com: Women’s History. 2007. 20 May, 2007. http://womenshistory.about.com/od/wangarimaathai/p/wangari_maathai.htm.

3.     “Wangari Maathai, The Nobel Peace Prize 2004.” The Nobel Foundation. 2004. 20 May, 2007. http://nobelprize.org/nobel_prizes/peace/laureates/2004/maathai-bio.html.

4.    “Wangari Maathai.” Wikipedia. May 2007. 20 May, 2007. http://en.wikipedia.org/wiki/Wangari_Maathai.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post