Kwa watumiaji wa Blackberry mtakuwa mnafahamu vyema kwamba simu za Blackberry zinavifurushi vyake spesho vinavyotambulika kama blackberry internet service (BIS) ambovyo ni tofauti na vifurushi vingine.
Jambo hili kuna baadhi ya watu linawachukiza, hata mimi kipindi natumia Blackberry nilikua nauzika, lakini nimeshajua jinsi ya kufanya. Naomba nikupe maujuzi kama ifuatavyo. Cha msingi ni kufuata taaratibu kama zinavyoelezwa
- Kwanza kabisa hakikisha simu yako ya blackberry haina bando spensheli (BIS). Unganisha bando la kawaida (lile ambalo kila mtu anaweza jiunga, lenye dakika, sms na MB/GB).
Inapopatikana TCP/IP Katika SImu Ya Blackberry
- Anza kwa kuweka alama ya tiki katika neno ‘ APN Setting Enabled‘ kisha mbele ya neno APN: andika internet , sehemu ya password na username paache bila kujaza kisha ‘save’ mabadiliko hayo.
Eneo la Kuweka APN Mpya Katika Simu Ya Blackberry
- Baada ya hapo utakua tayari umeshaunganisha internet kwa mfumo wa kawaida katika simu yako ya blackberry lakini kuna jambo moja muhimu la kufanya.. Nalo ni kuziruhusu Apps mbalimbali kutumia intaneti hiyo
- kwanza nenda eneo la ‘Options ‘ kisha tafuta ‘Application Management‘ kisha chagua Apps unazotaka kuziruhusu kutumia intanenti hiyo
Application Management ya blackberry
- Bofya App (kwa mfano WhatsApp) ukiwa ndani ya Application management kisha ‘ View Permissions ‘
- Bonyeza hilo neno ‘ View Permissions ‘ na kisha weka ‘Allow ‘ katika vipengele vitatu vitakavyotokea
Sehemu Ya Kuchagua Vitu Gani App Ifanye/Itumie
Baada ya kufanya yote hayo kwa mtiririko ‘save’ mabadiliko hayo kisha ‘resart’ simu yako. Kurestart simu yako kirahisi bofya ALT na SHIFT ya upande wa kulia pamoja na DEL kwa wakati mmoja bila kuachia mpaka simu yako itakapojizima. Baada ya sejunde kadhaa itawaka na utaweza kutumia App zako kama kawaida kwa kutumia intaneti ya kawaida.
Mara nyingi hata baada ya kutumia njia hii bado ‘ internet browser ‘ (Kivinjari cha blackberry) huwa kinagoma /kinasumbua kufanya kazi. Cha msingi kabla ya kuanza kutumia njia hizi hakikisha kwanza umeshusha kivinjari cha opera mini katika simu yako maana utakifanyia maboresho kama App zingine baada ya kufuata njia hizo
N.B:: Kwa kutumia njia hizi kupata internet, lakni hautaweza kutumia APP ya BBM kwani hiyo inatumika tu pale unapokuwa na kifurushi cha blackberry
Chanzo: tricksage.com