Msemaji wa polisi kutoka mkoa wa Tabora alisema Margareth Khamis, mwenye umri wa miaka 6, alitekwa nyara siku chache zilizopita katika kijiji cha Kona nne wilaya ya Nzega anapoishi na mama yake Joyce Mwandu na ndugu zake watatu.
Mwandu, alisema kundi la watu walioziba nyuso zao waliingia ndani ya nyumba yake na kumkamata binti yake na kukimbilia vichakani.
Juma Bwire, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, alisema operesheni ya kumkamata mtu aliyefanya kitendo hicho ilianza baada ya kupata fununu ya kusikia kwamba kuna mtu anataka kumnunua msichana huyo kwa bei waliyokubaliana.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka huduma ya kwanza ilisema kuwa mganga huyo alikubali kulipia shilingi 75,000 kwa viungo vya zeruzeru huyo.