Kila tunda lina umuhimu wake katika mwili wa binadamu na leo utafahamu faida mbalimbali kuhusu tunda la tangoMiongoni mwa faida tunazozipata kwa kula matango ni hizi zifuatazo:
FAIDA ZA MATANGO.
Matango huondoa harufu mbaya kinywani. Kwa kukiweka kipande cha tango mdomoni kwa dakika kadhaa, huuwa bakteria mbalimbali wanaosababisha magonjwa mbalimbali ya kinywa na harufu mbaya mdomoni.
Ulaji wa matango husaidia kuboresha kiwango cha maji ambayo huitajika mwilini, hii ni kutokana na matango kuwa na kiwango kikubwa cha maji. Maji haya husaidia kuondoa taka mwili pamoja na sumu mbalimbali ambazo miili yetu huzipata kupitia vyakula, madawa na hata vinywaji.
Inasaidia kupunguza (hangovers),uchovu, pamoja na hali ya kujisikia vibaya kutokana na unywaji wa kilevi. Hii ni kutokana na kuwa na vitamini B na maji mengi ambapo, baada ya mtu kunywa kilevi na kisha akaja kula matango kabla ya kulala, itamfanya asubuhi akiamka awe fresh na kuendelea na majukumu mengine.
husaidia katika mmeng’enyo wa chakula, matatizo ya tumbo kama vile kuvimbiwa, tumbo kujaa gesi, vidonda vya tumbo na mengineyo.
Yanasaidia kuondoa msongo wa mawazo. Matango yana kiwango kikubwa cha vitamini B ambayo husaidia kuboresha utendaji kazi wa mishipa mbalimbali ya fahamu mwilini na hivyo kuondoa hatari ya mtu kuathirika na msongo wa mawazo unaosababishwa na maisha ya kila siku.
Matango husaidia kuondoa hatari ya mtu kupata kansa. Yana kiwango kikubwa cha virutubisho vyenye asili ya mimea viitwavyo, lignans, ambavyo pamoja na vitamini c, husaidia kuondoa sumu mbalimbali na kuiboresha kinga ya mwili na hivyo kuepusha hatari ya mtu kupata kansa.