Baadhi ya mabaki ya ndege ya Ujerumani aina ya Airbus A320 baada
ya ajali.
Helkopta ikielekea eneo la tukio kuendelea na uchunguzi.
ZOEZI
la utafutaji miili ya watu 150 waliopoteza maisha katika ajali
ya
ndege
ya Ujerumani aina ya Airbus A320 yenye namba za
usafiri 4U 9525
iliyoanguka jana katika Milima ya Alps, Ufaransa limeendelea
leo huku
kifaa cha kunasia sauti kikipatikana huku kikiwa kimeharibika.
Vikosi vya uokoaji vikiwa eneo la tukio.
Waziri
wa maswala ya ndani nchini Ufaransa, Bernard Cazeneuve,
amesema
kuwa
kifaa hicho cha kunasa sauti kwenye ndege kilipatikana
jana Jumanne
baada ya kuanguka kwa ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Ujerumani
ikitokea
Hispania.
Mabaki ya ndege hiyo yaliyokutwa eneo la ajali.
Mbali
na kuharibika, Waziri Cazeneuve amesema kuwa kifaa hicho bado
kitatoa
taarifa kwa wataalam wanaojaribu kubaini kilichosababisha
kuanguka
kwa
ndege hiyo, ambayo iliwauwa abiria na wahudumu waliokuwemo
kwenye ndege
hiyo.
Helikopta zimeonekana zikipaa katika eneo la tukio huku maofisa wa
polisi wakiendelea kuchunguza mabaki ya ndege hiyo.
Sehemu ya kinasa sauti cha ndege hiyo.
Maofisa
wakuu wanaonya kuwa kupata mabaki ya miili ya abiria
itachukua
muda
mrefu kutokana na hali mbaya ya anga katika eneo hilo.
Kansela wa Ujerumani pamoja na Rais wa Hispania na waziri
wake mkuu, wanatarajiwa kuzuru eneo la ajali hiyo leo Jumatano.