Header ads

Header ads
» »Unlabelled » HII NDO LIST YA WATU MAARUFU KUTOKA KENYA NA TANZANIA, AMBAO WAMETAJWA NA MTANDAO WA KENYA KUA NI MAFREEMASON. WOLPER NAE KATAJWA

Inawezekana kila kitu kina wakati wake, kuna muda watu walikuwa wakisikia neno ‘Freemason’ ama ‘Illuminate’ kama inavyojulikana nchini Kenya wengi walikuwa wanaiona ni habari kubwa, lakini kwa sasa hivi inaweza kuchukuliwa kama sio big deal.

Sababu ni ile ile kuwa wengi wanaoendelea kwa haraka ama kuwa juu katika kile wanachokifanya basi utasikia huyo ni member wa Freemason, kwa upande wa Marekani wanasema ‘he/she just sold her/his soul to the devil’.  Japo kwa upande wa Marekani wapo wanaokiri kufanya hivyo kweli, ila kwa Africa Mashariki hakuna msanii aliyewahi kukiri.

Lakini yote hayo ni kama yanakanganya na kuonekana kama hayana mantiki hasa pale ambapo vithibitisho vya kinachoongelewa huwa havileti mantiki ya moja kwa moja. Pengine watu wanatafuta pesa kwa bidii na kumuomba Mungu lakini kwa kuwa kwenye mstari wa juu wanajikuta wanahisiwa kuwa member wa secret society (Freemason). Oh..au labda ndo vile kwa upande mwingine lisemalo lipo na kama halipo laja !

Tunathubutu kuziita blaa blaa kwa upande mwingine, lakini tukiweka kwenye mabano kuwa inaweza kuwa na ukweli, who knows!

Mtandao wa malimwengu wa nchini Kenya huenda ukawa na mfano mzuri wa kile nilichokitaja hapo juu, mtandao huo kupitia mwandishi wake imetaja majina ya wasanii wa Tanzania na Kenya wanaosemekana kuwa ni wafuasi wa Freemason, lakini kizuri zaidi ni kwamba mtandao huo umejaribu kuonesha vithibitisho na kushindwa kupata jibu la moja kwa moja kwa nini wasanii hawa wamekumbwa na hili. Inabaki hivyo hivyo kuwa tetesi tu.

Hawa ni wasanii waliotajwa na maelezo yanayowahusu:

TANZANIA:

1.Naseeb Abdul Jumaa (Diamond Platinum)
Picha aliyopiga mwaka jana akiwa na mzungu anaeaminika kuwa ni moja kati ya viongozi wa Freemason wakiwa wameweka pozi na kuonesha ishara inayooaminika kuwa ni ya Freemason, na kwamba alipoulizwa yeye alisema hakufahamu kama alikuwa anaelekezwa kupiga picha kwa pozi la ki-freemason. Kwa mujibu wa mwandishi anaona inaweza kuwa kweli kwa sababu anaonekana kuenjoy! 

2.Ali Kiba
Iliwahi kusemekana pia kuwa Ali Kiba ni Freemason, na wewe pia unaweza kufikiria sababu kwamba eti alikuwa maarufu sana na baadae kufifia. Maoni ya mwandishi (Hakuna uthibithibisho/ushaidi unaoweza kuwekwa thidi yake).
   
3.Jacquelin Wolper


Ni muigizaji maarufu wa kike mtanzania. Maoni ya mwandishi ( Hakuna ushaidi, tetesi peke yake hazina umuhimu)

KENYA:

1.Camp Mulla
Maoni ya mwandishi (Hapana, sio kweli. Sababu ya kufanikiwa kwenye muziki haimaanishi kuwa ni members wa Freemason. Hakuna mtu mwenye ushahidi kuwa Camp Mulla ni members wa Freemason).

2.Octopizzo
Maelezo yanayomhusu yanaonekana kuwa mengi sana kama kawaida, ni moja kati ya wasanii ambao tetesi za kuwa illuminate ni nyingi zaidi.

3.Nonini
Ukimtaja Nonini kama Illuminati lazima kitu serious zaidi kiandikwe ama ikielezwe. Nonini sio Illuminati (maoni ya mwandishi).

Hao ndio waliandikwa na kutolewa maoni ama maelezo na muandishi wa mtandao huo. Lakini tetesi huwa nyingi na kuongezeka mara kwa mara kwani hata Avril pia huwa anatajwa kuwa Illuminati na kwamba kazi yake ni kueneza usagaji nchini humo na eti sababu mojawapo ni mashairi ya wimbo wake ‘Chokoza’.

Haya yote yanasemwa tu, cha kufanya ni kile alichokisema Prof. Jay kwenye wimbo wake ‘Bongo Dar es Salaam’...  “Akili kumkichwa, ukizubaa unaachwa feli”.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post